Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo,akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa tasnia ya pamba uliowakutanisha viongozi wa serikali, wataalam wa kilimo pamoja na wakulima kutoka maeneo mbalimbali kujadili changamoto na fursa zilizopo katika sekta hiyo uliofanyika leo Aprili 16,2026 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde,akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa tasnia ya Pamba uliowakutanisha viongozi wa serikali, wataalam wa kilimo pamoja na wakulima kutoka maeneo mbalimbali kujadili changamoto na fursa zilizopo katika sekta hiyo uliofanyika leo Aprili 16,2026 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba (TCB), Christopher Gachuma,akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa tasnia ya Pamba uliowakutanisha viongozi wa serikali, wataalam wa kilimo pamoja na wakulima kutoka maeneo mbalimbali kujadili changamoto na fursa zilizopo katika sekta hiyo uliofanyika leo Aprili 16,2026 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa wadau wa tasnia ya pamba uliowakutanisha viongozi wa serikali, wataalam wa kilimo pamoja na wakulima kutoka maeneo mbalimbali kujadili changamoto na fursa zilizopo katika sekta hiyo uliofanyika leo Aprili 16,2026 jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emanuel Cherehani,akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara,wakati wa mkutano wa wadau wa tasnia ya Pamba uliowakutanisha viongozi wa serikali, wataalam wa kilimo pamoja na wakulima kutoka maeneo mbalimbali kujadili changamoto na fursa zilizopo katika sekta hiyo uliofanyika leo Aprili 16,2026 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Mzalendo blog-DODOMA
Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo,amesema dhamira ya Serikali ni kuifanya sekta ya pamba kuwa nguzo muhimu ya uchumi kwa kuongeza thamani ya zao hilo kupitia usindikaji wa ndani na kuimarisha masoko ya uhakika kwa wakulima.
Pia kuongeza uzalishaji, hatua kubwa inayolengwa sasa ni kuhakikisha pamba inayozalishwa nchini inachakatwa hapa hapa ili kuongeza ajira na mapato ya taifa.
Waziri Chongolo ameyasema hayo leo Aprili 16,2026 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wadau wa tasnia ya pamba uliowakutanisha viongozi wa serikali, wataalam wa kilimo pamoja na wakulima kutoka maeneo mbalimbali kujadili changamoto na fursa zilizopo katika sekta hiyo.
Chongolo amesema kuwa serikali inafanya kazi kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuvutia uwekezaji katika mnyororo mzima wa thamani wa pamba kuanzia shambani hadi viwandani.
“Nawaomba wadau wa sekta hii kushirikiana kwa karibu na serikali katika kuhakikisha wanatatua changamoto zilizopo, ikiwemo masuala ya bei, pembejeo na masoko, ili kufikia malengo ya kuongeza tija na kuinua maisha ya wakulima.”amesema Chongolo
Hata hivyo amesema kuwa uwekezaji katika viwanda vya nguo na usindikaji wa pamba utasaidia kupunguza utegemezi wa soko la nje ambalo limekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya bei.
Amesema hatua hiyo itaongeza ushindani wa zao la pamba la Tanzania katika soko la kimataifa huku ikihakikisha wakulima wananufaika zaidi na kazi yao kupitia bei nzuri na soko la uhakika.
Aidha, Waziri Chongolo amesisitiza umuhimu wa kuimarisha vyama vya ushirika ili viweze kusimamia vyema ukusanyaji na uuzaji wa pamba kwa uwazi na ufanisi zaidi.
“Dhamira ya serikali ni kuwainua wakulima wa pamba ili waweze kulima kwa tija na hatimaye kupata maendeleo endelevu nchini.”amesema
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba (TCB), Christopher Gachuma, amesema kuwa changamoto ya bei ndogo ya pamba inachangiwa kwa kiasi kikubwa na utegemezi wa soko la kimataifa.
Ameeleza kuwa kwa sasa bei ya pamba duniani iko chini, hali inayowaathiri moja kwa moja wakulima wa ndani. Kutokana na hilo, ameishauri serikali kuongeza uwekezaji katika viwanda vya ndani vya kuchakata pamba ili kupunguza utegemezi huo na kuongeza thamani ya zao hilo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Pamba Tanzania, Marco Mtunga, amesema serikali imeendelea kuimarisha tafiti za mbegu bora za pamba. Amefafanua kuwa mbegu zenye vinasaba kutoka Pakistani zimeonesha mafanikio makubwa katika kudhibiti wadudu waharibifu aina ya jassids, jambo linaloweza kuongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.
Mtunga ameongeza kuwa eneo la kilimo cha pamba limeongezeka hadi kufikia ekari 130 kutoka ekari 40 za msimu uliopita, ikiwa ni ishara ya mwitikio chanya wa wakulima. Pia, serikali imefanikiwa kusimika kiwanda cha kuchakata mbegu za pamba, hatua inayotarajiwa kuongeza ubora na upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima.
Akizungumzia mbinu bora za kilimo, Mtunga amesisitiza umuhimu wa wakulima kuzingatia ushauri wa kitaalamu, ikiwemo kupanda kwa kufuata viwango vinavyopendekezwa. Amesema shamba linapaswa kuwa na miche 44,444 kwa ekari, tofauti na mazoea ya kusia kiholela yanayosababisha idadi ndogo ya miche kati ya 5,000 hadi 10,000, hali inayopunguza tija.
Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emanuel Cherehani, amesema ipo haja ya kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha wakulima kupata mikopo na huduma za kifedha kwa urahisi, ili waweze kuwekeza zaidi katika kilimo cha pamba.
“Naiomba serikali kuweka mfumo madhubuti na wa haki katika ununuzi wa pamba. Amesisitiza kuwa kuwepo kwa mfumo mmoja ulio wazi na wenye tija kwa pande zote wakulima na wanunuzi kutasaidia kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kutokana na mifumo iliyopo sasa.”amesema Mhe.Cherehani.