Featured Kitaifa

SERIKALI YAIMARISHA MLOGANZILA KUWA KITOVU CHA ELIMU NA HUDUMA ZA TIBA

Written by Alex Sonna

 Serikali imedhamiria kuwa Kampasi ya Mloganzila ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) itakuwa mji wa kitaaluma na tiba, ikijumuisha vituo vya umahiri vitakavyotoa huduma za matibabu, elimu na utafiti ili kuimarisha sekta ya afya na elimu ya juu nchini.

Hatua hiyo, inatokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea katika Kampasi hiyo, pamoja na uwepo wa kituo cha umahiri cha magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ambacho ni cha Kipekee Afrika Mashariki.

Ameongeza kuwa Serikali imetenga dola za Marekani milioni 83 kwa ajili ya kujenga hospitali ya tiba ya magonjwa hayo ikiwa ni sehemu ya Kituo hicho ili kuwezesha kufanya utafiti kutoa mafunzo kwa vitendo na pia huduma kwa wagonjwa.

Aidha, Serikali imekamilisha mkakati wa kuanzisha kituo cha umahiri cha tiba ya kinywa na meno cha Afrika Mashariki .

Akizungumza Machi 17,2026 jijini Dar es Salaam katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ameeleza kuwa, juhudi hizo zinatokana na maono ya Mhe. Rais kuifanya Tanzania kuwa kitovu na taaluma za tiba katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na pia kuhakikisha kama Taifa linazalisha wataalamu na wabobezi wa kutosha kuhudumia watanzania wageni kutoka nje wanaokuja kupata huduma.

‘‘’Lengo ni kufanya Kampasi ya Mloganzila kuwa na vituo vingi vya umahiri katika nyanja mbalimbali za tiba na tofauti ya vituo hivi na hospitali ni kwamba, vitafanya utafiti, mafunzo na kutoa huduma ya tiba, ” Amesema Waziri Mkenda.

Prof. Mkenda ameongeza kuwa, Serikali pia inapanga kuanzisha kituo cha umahiri cha matibabu ya saratani ili kupanua wigo wa huduma za kibingwa nchini.

Kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kampasi ya Mloganzila imepatiwa zaidi ya shilingi bilioni 77 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Utawala Ndaki ya Tiba, Jengo la TEHAMA na Maktaba, maabara, kumbi za mihadhara, jengo la Anatomia na hosteli ya wanawafunzi ambapo kwa ujimla kampasi hiyo itachukua wanafunzi zaidi ya 1000.
[19:33, 17/03/2026] Liy Elimu: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko amekitaka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS) kwa kushirikiana na Wizara kutangaza kuongeza kasi ya kuitangaza Kampasi ya Mlonganzila kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanyika.

Mhe. Sekiboko ametoa rai hiyo Machi 17, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwenye mradi wa ujenzi katika Kampasi ya Mloganzila.

Amesema kazi iliyofanyika ni kubwa na kwamba nchi inakwenda kuzalisha wataalamu wabobezi katika maeneo mbalimbali ya tiba hivyo ni vizuri kampasi hiyo ikafahamika kwa elimu inayokwenda kuitoa lakini kwa kazi iliyofanyika kukiboresha na kuongeza fursa za mafunzo na tafiti.

Akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa majengo katika Kampasi ya Mloganzila unaogharibu zaidi ya Shilingi Bilioni 77 amesema
unakwenda vizuri ukiwa asilimia 80 na kwamba Kamati imeridhishwa na kasi na ubora wa kazi.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutaleta manufaa makubwa, ikiwemo kuongeza udahili wa wanafunzi, pamoja na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Amesisitiza kuwa upanuzi wa Chuo cha MUHAS unakwenda kupunguza uhaba wa madaktari na wataalamu afya nchini.

Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya Afya (MUHAS), Profesa Emmanuel Balandya, amesema eneo la Kampasi hiyo lina jumla ya ekari 3,800 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu mkubwa wa kimkakati na mingine.

Profesa Balandya ameongeza kuwa kukamilika kwa miundombinu hiyo kutaimarisha shughuli za ufundishaji, utafiti sambamba na utoaji wa huduma za kibingwa katika maeneo mbalimbali, ikiwemo magonjwa ya moyo na mishipa ya damu na mishipa ya fahamu

Naye Msimamizi Msaidizi wa Mradi wa HEET katika Chuo cha Muhas, Profesa Nathanael Siliri, amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa Kampasi ya Mloganzila ni kuifanya kuwa mji mkuu wa kitaaluma wa tiba, wenye vituo vya umahiri vitakavyotoa huduma za hali ya juu na kufanya tafiti zitakazosaidia maendeleo ya sekta ya afya nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.

About the author

Alex Sonna