Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Katimba (Mb), leo Januari 19, 2026,Mtumba, Jijini Dodoma, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Burundi nchini Tanzania, Mhe. Leontine Nzeyimana ambapo mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Burundi katika sekta ya Sheria.
Akizungumza katika mazungumzo hayo, Mhe. Katimba ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania ina dhamira ya dhati ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili katika nyanja mbalimbali, ikiwemo sekta ya Sheria, kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.
Kwa upande wake, Balozi wa Jamhuri ya Burundi nchini Tanzania, Mhe. Leontine Nzeyimana, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha uhusiano mzuri wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili, na kueleza kuwa Serikali ya Burundi iko tayari kuimarisha ushirikiano wa karibu katika sekta ya Sheria, ikiwemo kubadilishana uzoefu, kwa manufaa ya mataifa yote mawili.
