Polisi Kata ya Iyula, Mkaguzi wa Polisi Yakobo Dungumaro, ambaye pia ni Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi Iyula kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe, amewataka wananchi wa kata hiyo kuachana na migogoro ya kifamilia, akieleza kuwa migogoro hiyo husababisha chuki, visasi na kuvuruga mahusiano mema baina ya wanafamilia na jamii kwa ujumla.
Akizungumza Januari 13, 2026 wakati wa shughuli za maendeleo zilizofanyika katika Shule ya Sekondari Iyula Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe Mkaguzi Dungumaro alisema kuwa migogoro ya kifamilia imekuwa chanzo kikuu cha matukio mengi ya uhalifu, ikiwemo ugomvi, vurugu na uvunjifu wa amani, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia njia za amani katika kutatua migogoro yao kwa kushirikisha viongozi wa familia, wazee wa mila pamoja na Jeshi la Polisi pale inapobidi, badala ya kuchukua sheria mkononi.