Featured Kitaifa

RC CHALAMILA AFUNGUA MAFUNZO YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MKUU WA MKOA – DSM

Written by Alex Sonna

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Disemba 11, 2025 amefungua mafunzo kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya kinondoni.

RC Chalamila akifungua mafunzo hayo amesema kwamba chombo hicho au Baraza la Wafanyakazi ni muhimu katika utendaji wa Serikali na Taasisi zake, uwepo wa mabaraza haya ni utekelezaji wa sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2007 sura 366 na Sheria ya Utumishi wa Umma sura 298 pamoja na kanuni za kudumu katika Utumishi wa Umma toleo la tatu la mwaka 2009

“Baraza hilo ni chombo cha mawasiliano na kiungo muhimu kati ya menejimenti na wafanyakazi hivyo kupitia mafunzo haya mtakwenda kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo wajibu na majukumu ya Baraza la Wafanyakazi” Alisema RC Chalamila.

Aidha RC Chalamila ametoa pole kwa watumishi wote kufuatia madhara yaliyotokana na uvunjifu wa amani Octoba 29 ambapo amewataka watumishi kuwa mabalozi wazuri wa amani pia amewataka kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uaminifu.

Kwa upande wa katibu wa TUGHE Bi Sara Rwezaura Mkoa amesema kupitia mabaraza ya wafanyakazi husaidia kutatua changamoto mbalimbali za watumishi na kuwafanya watumishi kufurahia utumishi wao ambapo amepongeza Ofisi ya RAS DSM kufanya mafunzo hayo na kuzitaka Taasisi mbalimbali kuiga mfano huo.

Mwisho Mkuu wa Mkoa amewataka wafanyakazi ambao ni wanufaika wa mafunzo kutumia fursa hiyo kufuatilia na kuzingatia mafunzo yatayotolewa kwa kuwa yatakuwa nyezo au zana za kazi katika utendaji kazi kwa ufanisi.

About the author

Alex Sonna