Featured Kitaifa

ISW YAENDELEA KUNG’ARA KWENYE TUZO ZA NBAA

Written by Alex Sonna

 

Naibu Mkuu wa Taasisi Mipango, Fedha na Utawala, Dkt. Zena Mnasi Mabeyo akipokea tuzo ya Uandaaji wa Hesabu kwa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu wa Sekta ya Umma (International Public Sector Accounting Standards (IPSAS), kundi la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania

Katika tuzo hizo Chuo cha Ustawi wa Jamii kimeibuka mshindi wa tatu,ikiwa ni mara ya nane mfululizo toka mwaka 2017 #isw inashika nafasi za juu kwenye mashindano hayo.

Naibu Mkuu wa Taasisi aliambatana na Mhasibu Mkuu, Aisha Kapande Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Ndani kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii.

Tuzo hizo zimetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) usiku wa tarehe 04/12/2025 katika ukumbi wa APC Bunju, jijini Dar es Salaam.


 

 

 

 

 

About the author

Alex Sonna