Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali inalenga kuimarisha bajeti ya sekta ya elimu kutoka shilingi Bilioni 864 hadi kufikia shilingi Trilioni 1, ameyasema hayo leo tarehe 05 Disemba 2025 katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Jumuiya ya Walimu Wakuu wa Skuli za Sekondari za Zanzibar (JUWASEZA),
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Amesema Serikali itaendelea kuimarisha mazingira bora ya ufundishaji, maslahi na posho za walimu pamoja na ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuifanya Zanzibar kuwa na elimu bora
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akionge na kufungua Mkutano Mkuu wa 13 wa Jumuiya ya Walimu Wakuu wa Skuli za Sekondari Zanzibar (JUWASEZA), uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro, sambamba na uzinduzi wa dakhalia mpya ya wanafunzi wa kike wa skuli hiyo, iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, leo tarehe 05 Desemba 2025.
“Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akikata utepe kufungua dakhalia mpya ya wanafunzi wa kike ya Fidel Castro katika Mkoa wa Kusini Pemba, leo 05 Desemba 2025.
(PICHANI KUSHOTO) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mheshimiwa Lela Mohamed Mussa (WA PILI KUSHOTO) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba, Mberwa Hamad Mberwa (WA MWISHO KUSHOTO) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khadija Salum Ali;
(WA KWANZA KULIA) Mama Maryam Mwinyi, Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, na Mwenyekiti wa Zanzibar Maisha Bora Foundation;
(WA PILI KULIA) Mhandisi Zena Ahmed Said, Katibu Mkuu Kiongozi;
(WA MWISHO KULIA) Rashid Hadid Rashid, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.”
Muonekano wa Jengo la Dakhalia mpya ya wanafunzi wa kike ya Fidel Castro katika Mkoa wa Kusini Pemba,