Featured Kitaifa

KAMISHNA BADRU ATOA KONGOLE KWA TIMU ZA NGORONGORO ZILIZOSHIRIKI SHIMMUTA

Written by Alex Sonna

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bwana Abdul-Razaq Badru amezipongeza timu za Mamlaka hiyo zinazoshiriki mashindano ya Shirikisho la Mashirika ya serikali na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea mkoani Morogoro kwa kuendelea kulinda na kutangaza taswira ya taasisi hiyo kupitia sekta ya Michezo.

Akitoa salamu alipotembelea timu hiyo kwa niaba Kamishna Badru, Kaimu Meneja wa Uhusiano kwa umma bwana Hamis Dambaya amesema menejimenti ya Ngorongoro imeridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na timu hizo katika mashindano hayo na kulitangaza shirika kupitia utalii wa michezo (sport tourism)

Katika mashindano hayo Ngorongoro imefanikiwa kutwaa Medali saba huku ikidhihirisha upekee wake kimataifa na kuendelea kuwa Premium Safari Destination.

About the author

Alex Sonna