Featured Kitaifa

MCF NA VODACOM WATAMBULISHA MKOPO WA KIDIJITALI USIOHITAJI DHAMANA

Written by Alex Sonna

 

Taasisi ya Medical Credit Fund (MCF) kwa ushirikiano na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania wametambulisha  huduma mpya ya mikopo ya kidijitali ijulikanayo kama Afya Mkopo, inayolenga kuwawezesha watoa huduma za afya kupata mitaji bila kuweka dhamana.

Huduma hiyo inalenga vituo vya afya, famasia, kliniki, maabara pamoja na wauzaji wa vifaa tiba, ambapo kupitia mfumo wa LIPA NAMBA, taasisi hizo zitaweza kukopeshwa kwa haraka na kwa masharti nafuu ili kuboresha miundombinu, kupanua huduma na kuimarisha uendeshaji wa biashara.

Akizungumza wakati wa utambulisho  huo, Dkt. Heri Marwa, Mkurugenzi wa Nchi wa MCF, amesema mpango huo umebuniwa kuziba pengo la upatikanaji wa fedha salama na nafuu kwa biashara za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

 

Kwa upande wake,Bi. Delfina Thomas, Mshauri wa Mikopo ya Kidijitali, ameeleza kuwa Afya Mkopo inaleta uwazi, ufanisi na kasi katika upatikanaji wa mikopo, hatua itakayowasaidia watoa huduma kuwekeza kwa uhakika.

NayeBi. Hellen Kombo, Meneja wa Ripoti na Mipango kutoka Vodacom Tanzania, amebainisha kuwa matumizi ya LIPA NAMBA yameendelea kuongeza ujumuishaji wa kifedha, hivyo kuchochea maendeleo ya sekta ya afya nchini.

 

 

 

 

 

Picha zote na James Salvatory Torch Media 


About the author

Alex Sonna