Featured Kitaifa

MIXX YAZINDUA KAMPENI KUBWA YA “MAGIFT YA MIXX PESA” MWISHO WA MWAKA

Written by Alex Sonna

Kampuni ya huduma za kifedha, Mixx, leo imezindua kampeni kabambe ya mwisho wa mwaka iitwayo “Magift ya Mixx Pesa”, ikiwa ni hatua ya kuwashukuru wateja kwa kuendelea kuitumia katika huduma za kila siku.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Bi. Angelica Pesha, alisema kampeni hiyo inalenga kuleta hamasa kwa wateja katika msimu huu wa sikukuu ambao mara nyingi huambatana na mahitaji mengi ya kifedha.

 

Bi. Pesha alibainisha kuwa kupitia kampeni hiyo, wateja watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo milioni 1 kila siku, milioni 5 kila wiki, ushindi wa milioni 10 MixxMas, pamoja na Jackpot ya milioni 50 itakayokabidhiwa mwisho wa kampeni.

Amesema kuwa zawadi hizo ni uthibitisho wa jinsi Mixx inavyothamini uaminifu wa wateja wake, huku ikiongeza juhudi za kubuni huduma rahisi, nafuu na zinazowawezesha katika masuala ya malipo, akiba na huduma nyingine za kifedha.

Mixx imewahimiza wateja kutumia huduma zake kupitia mawakala, Mixx Super App, au kupiga *150*01# ili kupata nafasi ya kushinda na kuumaliza mwaka kwa mtindo kupitia kampeni ya “Magift ya Mixx Pesa”.

 

 

 

 

 

 

 

 

About the author

Alex Sonna