Featured Kitaifa

MAHUNDI ATAKA WAZAZI KUIMARISHA MALEZI CHANYA YA WATOTO

Written by Alex Sonna

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhandisi  Maryprisca Mahundi,akizungumza na vikundi vya malezi na wananchi kwa lengo la kuhamasisha malezi bora na kuwajengea uwezo kiuchumi wanachama wa vikundi hivyo  leo Novemba 27,2025  katika Kata ya Ihumwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Makundi Maalum, Sebastian Kitiku,akizungumza wakati wa Mkutano wa  vikundi vya malezi na wananchi kwa lengo la kuhamasisha malezi bora na kuwajengea uwezo kiuchumi wanachama wa vikundi hivyo  leo Novemba 27,2025  katika Kata ya Ihumwa jijini Dodoma.

Washiriki wa kikao wakimsikiliza Naibu  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhandisi  Maryprisca Mahundi (hayupo pichani) wakati akizungumza na vikundi vya malezi na wananchi kwa lengo la kuhamasisha malezi bora na kuwajengea uwezo kiuchumi wanachama wa vikundi hivyo  leo Novemba 27,2025  katika Kata ya Ihumwa jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhandisi  Maryprisca Mahundi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na vikundi vya malezi na wananchi kwa lengo la kuhamasisha malezi bora na kuwajengea uwezo kiuchumi wanachama wa vikundi hivyo  leo Novemba 27,2025  katika Kata ya Ihumwa jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhandisi  Maryprisca Mahundi, amewataka wazazi na walezi kote nchini kuimarisha malezi chanya na kuwalinda watoto dhidi ya changamoto za kijamii hususan ukatili wa mitandaoni, huku akisisitiza umuhimu wa kutumia fursa za uwezeshaji kiuchumi zinazotolewa na Serikali.

Mhandisi Mahundi ametoa  wito huo leo Novemba 27,2025  katika Kata ya Ihumwa jijini Dodoma, alipokutana na vikundi vya malezi na wananchi kwa lengo la kuhamasisha malezi bora na kuwajengea uwezo kiuchumi wanachama wa vikundi hivyo.

Mahundi amesema familia ndiyo msingi wa jamii yoyote na kwamba ni wajibu wa kila mzazi na mlezi kutafakari kama wanatimiza wajibu wao ipasavyo katika malezi, ulinzi na makuzi ya watoto.

“Ukweli ni kwamba wazazi na walezi wengi hatutimizi wajibu wetu kikamilifu, hususan katika malezi na makuzi ya watoto. Mtoto anayetarajiwa kuwa msaada wa familia na taifa anapaswa kulelewa tangu akiwa tumboni hadi kufikia umri wa miaka 18,” amesema Mhe.Mahundi

Aidha amesisitiza wajibu wa wazazi ni kutoa mahitaji ya msingi, kulinda mtoto dhidi ya ukatili, na kujenga mawasiliano ya mara kwa mara ili kuimarisha ukaribu (bond) utakaomwezesha mtoto kueleza changamoto anazopitia.

Hata hivyo  Mahundi ameonya kuwa ukosefu wa mawasiliano umewaacha watoto wengi wakiathirika na ukatili, ikiwemo unyanyasaji wa kingono, hali ambayo wazazi huibaini wakiwa wamechelewa.

Akizungumzia athari za teknolojia, amesema kuwa ukuaji mkubwa wa TEHAMA umeleta manufaa lakini pia umefungua mianya ya mmomonyoko wa maadili kwa watoto na vijana.

Kwa mujibu wa utafiti alionukuu, watoto 67 kati ya 100 wenye umri wa miaka 12–17 hutumia vifaa janja, huku watoto 4 kati ya 100 tayari wakikutana na ukatili wa mtandaoni, ikiwemo kurubuniwa kingono, kutishwa au kushawishiwa kutuma picha/video zisizofaa.

“Watoto wetu wako kwenye mazingira hatarishi mtandaoni. Wanahitaji uangalizi wa karibu na mwongozo wa maadili kutoka kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla,” amesisitiza.

Katika upande wa kiuchumi,  Mahundi amesema Serikali inaendelea kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kupitia usajili na mikopo nafuu inayotolewa na Benki ya NMB chini ya uratibu wa Maafisa Maendeleo ya Jamii, TEHAMA na biashara.

Tangu Februari 2024 hadi 26 Novemba 2025, jumla ya wafanyabiashara wadogo 115,035 wamesajiliwa, ambapo 44,336 tayari wamelipia vitambulisho vyao.

Kupitia vitambulisho hivyo, NMB imetoa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 9.8 kwa wanufaika 4,810 (2,619 wanawake na 2,191 wanaume).

Ametoa wito kwa viongozi wa vikundi kuongeza kasi ya usajili ili wanachama wengi zaidi wanufaike na mikopo hiyo nafuu.

Ametaja pia fursa nyingine za uwezeshaji kiuchumi kupitia mifuko 75 ya uwezeshaji—63 zikiwa za Serikali na 12 sekta binafsi—ikiwemo mikopo ya 10% ya Halmashauri, Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (uliofikisha Sh bilioni 1 kwa wanawake 150 hadi Novemba 2025), pamoja na zabuni za asilimia 30 chini ya Sheria ya Ununuzi wa Umma (2023) zinazotengwa kwa makundi maalum.

Vilevile ametaja  mikopo maalum kama Mwanamke Hodari ya Azania Bank, Impeju ya CRDB isiyo na riba, na mkopo wa Jasiri wa NMB wenye riba ya asilimia 14 kwa wanawake wamiliki wa biashara na asilimia 9 kwa miradi ya kilimo.

 Mahundi pia alizungumzia programu ya iSOKO inayotekelezwa na Wizara kwa kushirikiana na TWCC, akisema imekuwa daraja muhimu kwa wanawake kupata taarifa za masoko ndani na nje ya nchi kwa njia ya kidijitali.

Amewahimiza wanakikundi kuendelea kujikita katika kukuza uchumi wa kaya na kuifanya ajenda ya malezi kuwa ya kudumu katika vikao vyao vyote.

“Isiwe Mama analalamika baba hana muda na familia, au baba analalamika mama hana muda. Kutoa fedha pekee haitoshi; mawasiliano ni muhimu zaidi. Serikali itaendelea kuwa nanyi bega kwa bega katika kuwaelimisha na kuwawezesha,” amesema 

Aidha ameahidi kuwa Wizara itaendelea kutoa mafunzo na uhamasishaji endapo yatahitajika.

About the author

Alex Sonna