Featured Kitaifa

RAIS DKT MWINYI APOKEA KITABU MAALUM CHA HABARI PICHA ZA KAMPENI ZA UCHAGUZI 2025

Written by Alex Sonna

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea Kitabu Maalum chenye habari picha kutoka kwa Mkurugenzi wa Tahsil Solutions, Bw. Benny Kisaka, ambacho kina mkusanyiko wa taarifa za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar 2025 leo tarehe 20 Novemba 2025 Ikulu Zanzibar.

Dkt. Mwinyi amempongeza Mkurugenzi huyo kwa ubora na umakini uliotumika katika kukusanya taarifa na kutengeneza kitabu hicho.

Mkurugenzi wa Tahsil Solutions, Bw. Benny Kisaka, amefika Ikulu Zanzibar leo tarehe 20 Novemba 2025 kwa ajili ya kumkabidhi Rais Dkt. Mwinyi kitabu hicho, ambacho baadaye kitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, (PICHANI KULIA) Mohammed Hashim Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar

About the author

Alex Sonna