Na Sixmund Begashe – Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amekabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) tayari kwa kuiongoza Wizara hiyo yenye mchango mkubwa kiuchumi nchini.
Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo Novemba 20,2025, Mhe. Dkt. Kijaji licha ya kumpongeza mtangulizi wake kwa hatua hiyo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua kwenye nafasi hiyo, huku akiahidi kuwatumikia vyema nafasi hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Aidha aliekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana(Mb), amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini katika ngazi mbalimbali alizozitumikia na ameahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya wa Wizara hiyo pale itakapo hitajika.
Zoezi hilo la Makabidhiano limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Shani Kamala.
