Featured Kitaifa

CCM: HATUTASITA KUCHUKUA HATUA KALI KWA MAWAZIRI WAZEMBE

Written by Alex Sonna

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi,akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 19,2025 jijini Dodoma

Waaandishi wa habari kutoka Vyombo mbalimbali wakimsikiliza kwa umakini Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi,wakati akizungumza  leo Novemba 19,2025 jijini Dodoma

Na.Alex Sonna-DODOMA

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewakumbusha mawaziri na manaibu waziri walioapishwa jana kuwa kinatarajia utendaji wa juu na matokeo yanayoonekana, kikisisitiza kuwa hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya kiongozi yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Hayo yamesemwa leo Novemba 19,2025 jijini Dodoma na  Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi, amesema kuwa  uteuzi wa viongozi hao ni dhamana kubwa waliyopewa na Rais Samia Suluhu Hassan, hivyo hawapaswi kuichukulia kwa urahisi.

“Chama kinawataka mawaziri na manaibu waziri waende kufanya kazi kwa weledi na wasiende kumuangusha Rais. Wengi ni wapya, hivyo pamoja na kufurahia uteuzi, wakumbuke kuwa Rais hana mchezo. Anataka kazi, matokeo na utendaji uliotukuka unaozingatia utu kwa Watanzania wote,” amesema  Kihongosi.

Hata hi yo ameongeza kuwa CCM haitavumilia aina yoyote ya uzembe au kutozingatia maadili ya kazi katika Serikali inayotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho, akibainisha kuwa viongozi walioteuliwa wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, uwajibikaji na kwa kuwatumikia wananchi kama Taifa linavyotarajia.

“Chama cha Mapinduzi hakitasita kuchukua hatua kali kwa kiongozi yeyote mzembe ndani ya Serikali. Tunataka wote walioteuliwa waende wakawatumikie wananchi na si vinginevyo,” amesisitiza

About the author

Alex Sonna