Featured Kitaifa

MHANDISI SEFF AELEZA JITIHADA ZA TARURA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu Belem, Brazil

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amesema Serikali ya Tanzania imefanya jitihada kubwa ambayo imeweza kukamilisha miundombinu iliyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mengi.

Mhandisi Seff ameeleza hayo wakati akiwasilisha mada kwenye Mkutano wa Mkutano wa 30 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 30) unaoendelea katika Jiji la  Belem nchini Brazil.

Aidha, katika wasilisho lake Mtendaji Mkuu huyo aliweza kuonesha Makala fupi ya namna Wakala huo ulivyofanikiwa kurudisha mawasiliano ya miundombinu ya barabara iliyoharibika kwa kujenga miundombinu himilivu ‘resilient’ kwa athari za mabadiliko ya tabianchi na zenye uwezo wa kupitika mwaka mzima.

Amesema kupitia programu ya uondoaji vikwazo katika barabara (bottleneck), wameweza kujenga madaraja na barabara na hivyo kufungua mawasiliano katika vijiji na hivyo kuweza kuwasaidia wananchi kusafirisha mazao yao pia kuwarahisishia kupata huduma za kijamii zikiwemo huduma za afya.

Akichangia kwenye mradi wa Scale unaosimamiwa na TAMISEMI, amesema  TARURA ni mdau mkubwa kwenye mradi huo.

 

About the author

mzalendo