Featured Kitaifa

TANZANIA IKO TAYARI KUSHIRIKI MKUTANO WA UTALII DUNIANI

Written by Alex Sonna

Na Mwandishi Wetu, Riyadh

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, umewasili nchini Saudi Arabia kushiriki Mkutano Mkuu wa 26 wa Shirika la Utalii Duniani (UN TOURISM) unaofanyika mjini Riyadh.

Akizungumza katika kikao cha maandalizi na wataalamu wa Tanzania kilichofanyika katika Ubalozi wa Tanzania jijini hapa, Dkt. Abbasi amesema Tanzania ikiwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirika hilo, iko tayari kushiriki Mkutano huo muhimu ambapo pamoja na mambo mengine utamchagua Katibu Mkuu mpya wa Taasisi hiyo atakayeanza kazi rasmi Januari, 2026 akiwa na kazi ya kuchagiza maendeleo ya sekta ya utalii duniani.

About the author

Alex Sonna