Featured Kitaifa

DC NYAMWESE: HALI NI SHWARI HANDENI TUENDELEE KUPIGA KURA

Written by Alex Sonna

DC NYAMWESE: HALI NI SHWARI HANDENI TUENDELEE KUPIGA KURA

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, ameongoza wananchi wa Handeni kushiriki katika zoezi la upigaji kura leo, akibainisha kuwa hali ni shwari katika maeneo yote ya wilaya hiyo na kuwahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kupiga kura.

Akizungumza mara baada ya kupiga kura, Nyamwese amewahimiza wananchi ambao bado hawajapiga kura kujitokeza kabla muda haujaisha ili kushiriki kikamilifu katika mchakato wa demokrasia.

About the author

Alex Sonna