Featured Kitaifa

MNZAVA ASISITIZA AMANI SIKU YA UCHAGUZI

Written by Alex Sonna

 

Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Korogwe Vijijini, Timotheo Mnzava ameongoza mamia ya wananchi wa jimbo hilo katika mkutano wa kufunga kampeni huku akiwataka Watanzania wote kuepuka vishawishi vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani .

Akiomba kura za CCM na katika mkutano uliofanyika katika kata ya Mombo, Mnzava amewahimiza vijana na wananchi kwa ujumla waendelee kuilinda amani kwa wivu mkubwa iliyoasisiwa na viongozi wa taifa letu.

Mnzava alieleza wananchi namna ambavyo wasichezee amani mana mataifa mengine ambayo hayana amani watoto, wamama na wazee wanaishi katika mazingira hatarishi na kupoteza uhai wao.

“Amani hii inayotamkwa kwenye katiba yetu, inayotamkwa kwenye dini zetu tuifate na sote tuilinde kwa kushiriki uchaguzi kwa utulivu na amani”.

Aidha Mnzava amemuombea kura Mgombea wa Urais Dkt Samia Suluhu Hassan na wananchi wamemuahidi kumchagua kwa kura nyingi za heshima na kupita kwa kishindo.

Mnzava ameleza kuwa katika kipindi chake cha uongozi, miradi ya barabara, nishati, afya na elimu imepiga hatua kubwa, akibainisha kuwa zaidi ya asilimia 100 ya vijiji vyote 118 vya jimbo hilo sasa vimeunganishwa na umeme, huku barabara za kiuchumi zikijengwa.

About the author

Alex Sonna