Featured Kitaifa

π—ͺπ—”π—§π—”π—‘π—­π—”π—‘π—œπ—” π—ͺπ—”π— π—˜π—₯π—œπ——π—›π—œπ—žπ—” 𝗑𝗔 π—¨π—§π—˜π—‘π——π—”π—π—œ π—žπ—”π—­π—œ π—ͺ𝗔 π——π—žπ—§.π—¦π—”π— π—œπ—”-π——π—žπ—§. π—‘π—–π—›π—œπ— π—•π—œ

Written by Alex Sonna

-π˜Όπ™’π™¨π™π™ͺ𝙠π™ͺ𝙧π™ͺ π˜Ώπ™ π™©. π™Žπ™–π™’π™žπ™– 𝙠𝙬𝙖 𝙠π™ͺπ™šπ™£π™™π™šπ™‘π™šπ™– 𝙠π™ͺ𝙒π™ͺπ™–π™’π™žπ™£π™ž 𝙣𝙖 𝙠π™ͺπ™’π™©π™šπ™ͺ𝙖 𝙠π™ͺ𝙬𝙖 π™ˆπ™œπ™€π™’π™—π™šπ™– π™ˆπ™¬π™šπ™£π™―π™–.

MWANZA.

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema kuwa atahakikisha anamsaidia Mgombea Urais wa CCM kwa nguvu, akili, maarifa na uaminifu ili ndoto na maono yake na utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2025/30 yafanikishwe kwa mafanikio makubwa.

Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi wa Mwanza na maeneo jirani katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi za CCM, leo tarehe 28 Oktoba 2025, Dkt. Nchimbi alisema:

β€œNakushukuru sana Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama chetu cha CCM kwa imani yako kubwa kwangu kwa kunipendekeza kuwa msaidizi wako mkuu. Miaka minne iliyopita uliniteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, baadae ukanipendekeza kupitia vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, na sasa umeniamini katika nafasi ya Mgombea Mwenza.”

Aliongeza kuwa ndani ya kipindi cha miaka minne, Mgombea Urais wa CCM ameonyesha imani kubwa kwake kwa kumpa nafasi muhimu ndani ya Taifa na ndani ya chama.

β€œNakuhakikishia kuwa imani uliyoonesha, namna pekee ninayoweza kuilipa ni kukusaidia kwa nguvu, akili, maarifa na uaminifu ili ndoto na maono yako na utekelezaji wa ilani yetu ya CCM (2025/30) ufanyike kwa mafanikio makubwa katika miaka mitano ijayo,” alisema Dkt. Nchimbi.

Mgombea mwenza huyo pia alisema kuwa wananchi waliotembelewa katika sehemu zote wanapendekeza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/25 umewaridhisha kwa kishindo.

β€œWatanzania katika sehemu zote tulizopita wameridhika na utekelezaji wako wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/25 kwa kishindo na wametutuma tukueleze kuwa kesho watakupa kura nyingi za ushindi wa kishindo. Hilo linatokana na utendaji kazi wako katika Serikali ya Awamia ya Sita unayoiongoza inayotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM),” alisema.

About the author

Alex Sonna