Featured Kitaifa

MHANDISI MWAJUMA AWAELEKEZA WATUMISHI WIZARA YA MAJI KUFUATA SHERIA NA TARATIBU

Written by Alex Sonna

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, ameelekeza kazi zote katika wizara hiyo zifanyike kwa kuzingatia Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.

Amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala ya Wizara ya Maji, akisisitiza umuhimu wa uadilifu na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao.

“Ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa kila kazi inafanywa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa. Hii itasaidia kuimarisha utumishi bora na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi,” amesema Mhandisi Mwajuma.

Aidha,amesisitiza suala la kuzingatia mabadiliko yanayojitokeza katika mfumo wa utumishi wa umma na kutoa majibu kwa watumishi wanapokumbana na changamoto katika masuala mbalimbali.

“Watumishi wa umma wanapokosa kuelewa au kukabiliana na changamoto fulani, ni lazima tutoe mwongozo na msaada unaohitajika ili kazi ziendelee kwa ufanisi. Hii ni sehemu ya kuhakikisha tunatimiza malengo ya Wizara kwa ufanisi,” ameongeza.

About the author

Alex Sonna