Na Mwandishi Wetu WMJJWM- Njombe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Mkaundi Maaalum Dkt. John Jingu, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoani Njombe kutunza na kutumia kwa umakini pikipiki walizopewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha utendaji na utoaji huduma kwa wnanchi.
Dkt. Jingu amesema hayo tarehe 24 Oktoba, 2025 wakati wa hafla ya makabidhiano ya pikipiki nane (8) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa ngazi ya kata mkoani humo.
“Twende tukavitumie vifaa hivi kwa matumizi sahihi kwani ni hatua muhimu katika kuleta matokeo chanya katika jamii, hasa katika kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali” amesema Dkt.Jingu
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Judica Omari, ameishukuru Serikali kwa msaada huo huku akieleza kuwa pikipiki hizo zitaboresha utoaji wa huduma kwa wakati na kwa ufanisi zaidi.
“Kwa niaba ya Mkoa wa Njombe pamoja na Halmashauri zake zote, tunaishukuru Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum kwa jitihada kubwa katika kuboresha huduma kwa wananchi,” amesema Judica
Nao baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii waliopokea pikipiki hizo walieleza pikipiki hizo zitakuwa mkombozi wa changamoto waliokuwa wanakumbana nazo kwa muda mrefu, ikiwemo ugumu wa kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali.
