Featured Kitaifa

DKT. SERERA AIPONGEZA WRRB KWA USIMAMIZI BORA WA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI KARATU

Written by Alex Sonna

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya  kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.

Na Alex Sonna, Karatu

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera, ameipongeza Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) kwa kusimamia vyema mfumo wa stakabadhi ghalani unaotekelezwa katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha, akisema umeleta tija kubwa kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao.

Akizungumza baada ya kutembelea maghala yaliyopo katika eneo hilo, Dkt. Serera amesema lengo la ziara yake ni kujionea kwa karibu namna mfumo huo unavyofanya kazi pamoja na mwitikio wa wadau.

“Nimejionea na kujiridhisha kwamba mfumo huu unafanya kazi vizuri. Tutaendelea kuelimisha wadau zaidi ili wote watumie mfumo huu wenye faida nyingi kwa taifa,” amesema Dkt. Serera.

Amesema mfumo wa stakabadhi ghalani umeleta ushindani katika soko la bidhaa za kilimo na kuwawezesha wakulima kupata faida kubwa kutokana na bei nzuri za mazao yao.

“Maghala yetu mengi yamewekwa katika hali ya usafi wa hali ya juu. Hakuna mzigo unaoingia ghalani bila kusafishwa na kuandaliwa vizuri. Faida nyingine ni kuwa mfumo huu unahakikisha kila mzigo unapimwa kwa uzito unaostahili,” amesema.

Aidha, amesema Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo imejipanga kuhakikisha bidhaa zote zinazofika kwa mlaji zinakuwa salama na zenye ubora unaozingatia viwango vya usalama wa chakula, ili kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayotokana na matumizi ya vyakula visivyo salama.

Dk. Serera ametoa wito kwa wadau wa kilimo na biashara kuendelea kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani, huku serikali ikiendelea kushughulikia changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,  Asangye Bangu amesema mfumo huo umepokelewa vizuri na wakulima wa mbaazi wilayani Karatu, na kwamba umechangia kupatikana kwa bei nzuri ya zao hilo sokoni.

“Kwa msimu wa mwaka huu, Karatu imekuwa miongoni mwa maeneo yenye bei kubwa zaidi ya mbaazi nchini. Hii ni ishara ya mafanikio ya mfumo wa stakabadhi ghalani,” amesema.

Ameongeza kuwa Bodi inaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha sekta ya kilimo na kuweka mazingira rafiki ya biashara kupitia taasisi za wizara husika.

“Tunawahakikishia wanunuzi na watumiaji kwamba bidhaa zinazotolewa kupitia mfumo huu zina ubora unaoendana na thamani ya fedha zao. Mfumo huu unaleta uwazi, usawa na faida kwa pande zote,” amesisitiza.

Awali Mkusanya mali Bi.Gladness Tarimo,  amesema mfumo wa stakabadhi ghalani umeleta manufaa makubwa kwa vijana kwani umewapa nafasi ya kuuza bidhaa zao kwa bei shindani na inayojulikana wazi katika soko.

Naye, Evarist Silayo, Mfanyabiashara wa mazao ambaye kampuni yake inamiliki maghala katika maeneo matatu nchini ikiwemo Karatu, amesema mfumo huo umeondoa upunjaji na kuongeza uaminifu kati ya wakulima na wanunuzi.

“Kwa mfano, katika mnada wa kwanza uliofanyika hapa Karatu, bei ya mbaazi kwa kilo ilikuwa zaidi ya Sh.1,000, tofauti na bei ya awali iliyokuwa kati ya Sh.750 hadi Sh.800. Wakulima waliona faida kubwa ya kutumia mfumo huu,” amesema Silayo.,

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dkt. Lameck Karanga Ng’ang’a wakati wa ziara yake ya  kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza wakati wa ziara yake ya  kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,  Asangye Bangu, wakati wa ziara yake ya  kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akiendelea kukagua  na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akiendelea kukagua  na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya  kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya  kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,  Asangye Bangu,akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera (hayupo pichani) kwa  ziara yake ya  kutembelea na kujionea maghala yanayotumia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika Halmashauri ya Karatu, mkoani Arusha.

Mfanyabiashara wa mazao ambaye kampuni yake inamiliki maghala katika maeneo matatu nchini ikiwemo Karatu Evarist Silayo, akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wakulima nchini.

 Mkusanya mali Bi.Gladness Tarimo, akielezea jinsi mfumo huo unavyowasaidia katika kuinua kipatao chao.

About the author

Alex Sonna