Wakati ikiwa imesalia takribani siku 1O kabla ya Kufanyika kwa Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kupitia CCM, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi ametoa rai kwa Wakazi wa Lituhi, Jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma kutunza Vitambulisho vya kupigia kura kwa ajili ya kutimiza Wajibu wa kikatiba na Msingi ili kuchagua Viongozi watakaounda Serikali ijayo, ambayo itakuwa Chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan.
Dkt Nchimbi ametoa rai hiyo leo Oktoba 19, 2025 akiwa katika muendelezo wa Kampeni za Kusaka Kura za Ushindi wa Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Kunadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Sera zake ambazo pia zimelenga Kuboresha maisha ya Watanzania.
“Ndugu zangu Wana nyasa, nimekuja hapa kwa ajili ya Kuwahakikishia kwamba sitawaangusha, nitakuwa Msaidizi mzuri wa Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa hiyo nami niwaombe msiniangushe Ifikapo Oktoba 29, mjitokeze kwa Wingi kwenda kupiga kura na Kumchagua Dkt Samia Suluhu Hassan ili aweze kuongoza Serikali ijayo kwa Muhula wa miaka mingine mitano” amesema Dkt Nchimbi.