Featured Kitaifa

TANZANIA YAJIPANGA KUONGEZA UFANISI UKUSANYAJI WA MAPATO

Written by Alex Sonna

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Finance Ministers Meeting – CFMM) uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.

Na. Chedaiwe Msuya, WF, Washington.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban amesema kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na Jumuiya ya Madola, katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa rasilimali za ndani kupitia mifumo ya kisasa ya ukusanyaji kodi na ukaguzi wa forodha (IDRAS na TANCIS), pamoja na utekelezaji wa Mkakati wa Kipindi cha Kati wa Mapato.

Bi. Amina amesema hayo wakati akimwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika kikao cha Jukwaa la Kimataifa linalowakutanisha Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola, (Commonwealth Finance Ministers Meeting, CFMM 2025), kilichofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Aidha, alibainisha dhamira ya Tanzania ya kuendeleza uchumi wenye utofauti, ukiwa na uwekezaji katika utalii, teknolojia ya habari na mawasiliano, ubunifu wa kijani, na madini endelevu. Ushirikiano wa kibiashara na Ulaya, Asia na Mashariki ya Kati, pamoja na sera za kibiashara za kikanda na mikakati ya uwekezaji kutoka diaspora, unachukuliwa kuwa muhimu.

Bi Amina alimalizia kwa kuthibitisha dhamira ya Tanzania kushirikiana na wanachama wa Jumuiya ya Madola katika kufanikisha malengo ya uhimilivu wa kiuchumi, ukuaji jumuishi, na maendeleo endelevu, huku akisisitiza thamani ya msaada wa kiufundi na mazungumzo ya sera yanayopatikana kupitia jukwaa hili.

Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto za uchumi wa dunia, na kutafuta mikakati ya kuimarisha uhimilivu wa kiuchumi katika nchi wanachama.

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Finance Ministers Meeting – CFMM) uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akifuatilia Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Finance Ministers Meeting – CFMM) uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Dkt. Fred Msemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Kitaifa wa Tume hiyo, Bi. Angela Shayo, wakifuatilia Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Finance Ministers Meeting – CFMM) uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.

 

Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha wakifuatilia Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Finance Ministers Meeting – CFMM) uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Washington DC, Marekani)

About the author

Alex Sonna