Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila leo tarehe 15 Octoba 2025 amekagua miradi ya ujenzi wa madaraja na barabara Jijini Dar es salaam yenye gharama ya shilingi Bilioni 224.22 inayotekelezwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kumlaki Mhe Chalamila amemtaka wakandarasi wa miradi hiyo yote kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo haraka iwezekanavyo kwa muda uliopangwa.
RC Chalamila ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Daraja la Jangwani lenye urefu wa mita 390 pamoja na barabara unganishi (0.7km) linalojengwa na Mkandarasi M/s China Communications Construction Company Ltd kwa ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa uendeshaji wa Bonde la Msimbazi huku Mhandisi Mshauri ni M/s Leporogo Specialist Engineers ya Afrika Kusin iikishirikiana na Afrisa Co nsulting Ltd ya Tanzania na Dong Myeong Engineering Consultants &Architecture Co. Ltd ya Korea Kusini kwa gharama ya shilingi Bilioni 97.
Mhe Chalamila amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kuwalipa wakandarasi ili kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo kwa wakati uliopangwa kwa mujibu wa mkataba.
Rc Chalamila amebainisha kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutarahisisha huduma za wananchi kwani watanzania wanasubiri kwa hamu na shauku kubwa miradi hiyo pindi itakapokamilika kwani itakuwa kichocheo cha maendeleo ya mkoa na kuepusha vifo visivyo vya lazima.
Awali, akisoma taarifa ya miradi inayotekelezwa Mkoani Dar es salaam, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Alinanuswe Kyamba mbali na mradi wa ujenzi wa daraja la Jangwani ameitaja Miradi mingine inayoendelea kutekelezwa katika mkoa huo kuwa ni pamoja na Ujenzi wa daraja la Kigogo (50m) linalojengwa na mkandarasi M/S Kings Builders Ltd Kwa ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi Mhandisi Mshauri ambaye ni TECU kwa gharama ya shilingi Bilioni 17.76, Ujenzi wa daraja la Nguva katika barabara ya Mji Mwema – Kimbiji – Pemba Mnazi Road (R.795) na kalavati (Box) eneo la Mikadi katika barabara ya Kongowe – MjiMwema – Kivukoni Road (R.793) linalojengwa na Mkandarasi ni M/S Nyanza Road Works kwa ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa uendeshaji wa Bonde la Msimbazi huku Mhandisi Mshauri akiwa ni TECU kwa gharama ya shilingi Bilioni 9.217
Ujenzi wa daraja la Kisarawe II na Amani Gomvu, kalavati (Box Culverts) eneo la GetiJeusi katika barabara ya Kongowe – MjiMwema – Kivukoni Road (R.793) pamoja na ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua (3km) katika barabara ya Kigamboni – Kibada – Sangatini (R.798) unaojengwa na Mkandarasi M/S OSAKA Company Ltd kwa ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa uendeshaji wa Bonde la Msimbazi, Mhandisi Mshauri akiwa ni TECU na unajngwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 9.419
Serikali inaendelea na Ujenzi wa daraja la Mtongani katika barabara ya Kunduchi – Ununio – Boko Road (R.748) pamoja na ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua (5km) katika barabara ya Morocco – Africana, Mwenge – Mlalakuwa (MwaiKibaki Road) unaojengwa na Mkandarasi ni M/S Shandong Luqiao Group Co. Ltd (China) kwa ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa uendeshaji wa Bonde la Msimbazi) ambapo Mhandisi Mshauri ni TECU na mradi huo unajengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 24.656.
Kadhalika mradi mwingine ni Ujenzi wa Daraja la Mkwajuni (20m) katika barabara ya Kawawa linajengwa na Mhandisi ni M/S Kings Builders Ltd kwa ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa uendeshaji wa Bonde la Msimbazi na Mhandisi mshauri ni TECU ukiwa unajengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 11.614 pamoja na mradi wa upanuzi wa barabara ya Mbagala Rangi Tatu – Kongowe yenye urefu wa kilomita 3.8 pamoja na daraja la mzinga kwa gharama ya shilingi Bilioni 54.6