WAZIRI Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, amefariki dunia leo Jumatano 15,2025 akiwa na umri wa miaka 80.
Taarifa zinaeleza kuwa kiongozi huyo wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM)amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali moja nchini India.
Kifo chake kimetokea wiki chache baada ya kuzagaa tetesi mitandaoni zilizodai kuwa alikuwa katika hali mahututi, madai ambayo familia yake ilikuwa imekanusha vikali.
Awali, kaka yake mkubwa ambaye pia ni Seneta wa Siaya, Dkt. Oburu Odinga, aliwahakikishia Wakenya kuwa Raila alikuwa anaendelea kuimarika kiafya na alikuwa akipata nafuu nchini India.
Akizungumza na vyombo vya habari, Dkt. Oburu alikanusha taarifa zilizodai kwamba Raila alikuwa katika hali mbaya, akizitaja kuwa zimezidishwa na hazikuwa sahihi.