Featured Kitaifa

ADEM NA SHULE BORA WAZINDUA JUKWAA LA KITAIFA LA UONGOZI WA ELIMU

Written by Alex Sonna

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAKALA wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM pamoja na Programu ya Shule Bora wameshirikiana kuandaa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, hatua inayolenga kuimarisha ubora wa uongozi katika sekta ya elimu nchini.

Akizungumza leo Oktoba 3,2025 Mkoani Morogoro wakati akizindua jukwaa hilo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar amesema awali kutokana na kutokuwepo kwa jukwaa la pamoja maeneo mengi yalikosa huduma kutokana na taasisi kurundikana eneo moja ambapo kupitia jukwaa hilo litakomesha hali hiyo kwani maeneo yaliyonahuduma yatafahamika na maeneo yaliyokosa kufahamika hivyo kufungua fursa kwa maeneo mengine kupata huduma.

“Kuna baadhi ya maeneo unakuta yanakosa kupata huduma sababu watu wote wamekwenda sehemu moja sababu na hakuna mtu wa kuwaambia sasa kupitia jukwaa hili litawaambia nani anafanya nini na wapi”. Amesema.

Aidha amesema kuwa umuhimu wa jukwaa hilo unajikita katika Ajenda ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 na Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, toleo la mwaka 2023, ambazo zinatambua mchango wa uongozi wa elimu katika kuongeza ufanisi wa taasisi za mafunzo zinazolenga kuwaandaa vijana kwa stadi za ajira na kujitegemea.

“Uongozi wa shule unachangia takribani 27% ya matokeo ya wanafunzi, baada ya ufundishaji na ujifunzaji. Viongozi wa shule wanapaswa kuhakikisha kuwa uongozi wao unawaunga mkono walimu na wanafunzi”. Amesema

Amesema kuwa kwa kuwawezesha wakuu wa shule, maafisa elimu na wasimamizi, ADEM inahakikisha uongozi katika elimu unakuwa wa kitaaluma na pia chachu ya mabadiliko kwa mafanikio ya sekta ya elimu.

Amesema kupitia hilo, jukwaa litasaidia kuimarisha dhamira ya Wizara kuhakikisha elimu bora na uongozi thabiti katika ngazi zote za mfumo wa elimu.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo ADEM, Dkt. Emmanuel Mollel akizungumza kwa niaba ya Mtendaji mkuu wa ADEM, amezishukuru taasisi zilizojumuika katika Mkutano huo kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kutoa mafunzo ya uongozi ambapo pia amebainisha kuwa kupitia jukwaa hilo watajumika kufanya tafiti za pamoja ambapo zitasaidia kuyafahamu maeneo yenyeuhitaji.

Amesema ushirikiano huo utatoa nafasi ya kupata mafunzo maalum ya kimataifa katika uongozi na upangaji wa elimu ambayo kwa sasa hayapatikani kwa kiwango kikubwa nchini.

“Ushirikiano kati ya ADEM na mashirika yasiyo ya serikali pia utaimarisha maamuzi yanayotokana na ushahidi katika usimamizi wa elimu, kulinganisha juhudi za maendeleo ya uwezo nchini na viwango vya kimataifa, na kukuza taasisi kupitia kubadilishana ujuzi”. Amesema

Amesema ushirikiano huo utahakikisha kwamba maafisa elimu wa Tanzania wanakuwa na weledi zaidi katika kusimamia rasilimali, kufuatilia utekelezaji wa sera na kukabiliana na changamoto mpya katika sekta ya elimu.

Naye, Kiongozi wa Mradi wa Shule Bora, Bi. Virgin Briand, amesema usimamizi na uongozi madhubuti wa elimu ni nyenzo ya maendeleo na matokeo bora katika ufundishaji na ujifunzaji shuleni.

Amesema amesema kuwa mradi huo unachangia kuwezesha mafunzo ya kwa viongozi wa shule ili kuwajengea uwezo wa kupanga na kuongoza kimkakati na kukuza utamaduni bora wa kujifunza, huku Naibu Kiongozi wa Programu ya Shule Bora, Bw. Benjamin Oganga, akiongeza kuwa jukwaa hilo litawasaidia viongozi kuwa na weledi na maarifa ya kuimarisha elimu bora.

Vilevile, Mnufaika wa mafunzo ya uongozi na Usimamizi wa Elimu Bi.Tumaini Ruthless amesema mafunzo hayo ni mazuri katika uboreshaji wa elimu ambapo yamejumuisha elimu shirikishi na uongozi shirikishi ambapo yamemjenga kama kiongozi kushirikisha anaowaongoza katika kuboresha elimu nchini.

Mbali na hayo ameishauri serikali kuendelea kuwapatia mafunzo walimu nchini ili kuwajengea uwezo wa ufundishaji sambamba na kuboresha mazingira ya ujifunzaji yanayoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kwa kuwekeza katika rasilimali fedha,nguvu kazi sambamba na vifaa vya kujifunzia.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa ufundishaji na ujifunzaji wa Shirika la Opportunity Education, Bw. Laurent Gama amesema jukwaa hilo liloundwa na ADEM linawapatia wasaa kama wadau wa elimu kuangalia uwekezaji uliofanyika jinsi utakavyoleta matokeo chanya kwa jamii sambamba na kufanya uratibu wa matumizi bora wa rasilimali kwa kutambua maeneo yenye uhitaji sambamba na kufanya mashirikiano na taasisi nyingine.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.
iongozi wa Mradi wa Shule Bora, Bi. Virgin Briand, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.
Makamu Mkuu wa Chuo ADEM, Dkt. Emmanuel Mollel akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.

Kaimu Mkurugenzi Elimu ya Awali na Msingi – OR TAMISEMI, Ally Swalehe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 2025 mkoani Morogoro.

Mkurugenzi Elimumsingi – WyEST, Abdul Maulid akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 2025 mkoani Morogoro.

Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Dkt. Lucas Mzelela akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.

Baadhi ya wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu wakiwa katika uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa elimu nchini wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa elimu nchini wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa elimu nchini wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu 2025, ambao umefanyika leo Oktoba 3, 202( mkoani Morogoro.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

About the author

Alex Sonna