Featured Kitaifa

MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI RUKWA

Written by Alex Sonna

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati akimkabidhi mwenge wa uhuru mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Charles Nyerere katika kijiji cha kizi kata ya Paramawe wilaya ya Nkasi. 

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Charles Nyerere wakati akimkabidhi mwenge wa uhuru mkuu wa wilaya ya Nkasi Peter lijualikali

Na Neema Mtuka Sumbawanga.

Rukwa :Mwenge wa Uhuru umepokelewa rasmi katika Kijiji cha Kizi kata ya paramawe Tarafa ya Namanyere mkoa wa Rukwa  ukitokea mkoani Katavi ambapo  utakimbizwa kilomita 653.1 unatarajiwa kuzindua miradi 7 ,huku miradi 15 itawekewa mawe ya msingi na miradi 12 ikikaguliwa.

Awali akipokea mwenge wa uhuru mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Charles Nyerere amesema mwenge utakimbizwa kwa muda wa siku 4 katika wilaya 3 zenye halmashauri 4 ambazo ni Halmashauri ya wilaya ya Nkasi, Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya wilaya ya Kalambo na Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga.

Katika kipindi chote hicho Mwenge wa uhuru utatembelea miradi 34 ya maendeleo na klabu 8

“Miradi hii ina thamani ya sh Billion 55.3 ambayo itawekewa mawe ya msingi,itakaguliwa na kizinduliwa.

Ukiwa katika halmashauri ya Nkasi Mwenge wa uhuru utakimbizwa kwa umbali wa kilomita 153 na kupitia miradi ya maendeleo 08 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.

Ambapo tarifa hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali katika juhudi za kupambana na rushwa,dawa za kulevya na malaria.

“Tujali afya zetu kwa kuzingatia aina ya chakula tunachokula ili kuimarisha ustawi wa afya zetu na kuboresha hali ya lishe.”amesema Maklijualika. 

About the author

Alex Sonna