MGOMBEA urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, ameahidi kurejesha viwanda vya chai nchini ndani ya siku 100 endapo atachaguliwa kuingia Ikulu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Akihutubia wananchi wa mji wa Lupembe, mkoani Njombe, wakati akiendelea na kampeni zake, Mwalimu amesema kufa kwa viwanda ni sawa na kuua ukuaji wa uchumi wa taifa.
“Nchi yoyote ambayo inaua viwanda, tafsiri yake ni kuua ukuaji wa uchumi wa nchi,” amesema Mwalimu
Aidha amewaomba wananchi wa Lupembe wampe ridhaa ya kuongoza Tanzania.