Featured Michezo

DK.SAMIA:MSONGA KUJENGEWA UWANJA MKUBWA WA MICHEZO

Written by Alex Sonna

MGOMBEA wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa endapo ataaminiwa na wananchi kuunda serikali katika kipindi kijacho cha miaka mitano, ujenzi wa uwanja mkubwa wa michezo utafanyika Msoga, Chalinze mkoani Pwani.

Akihutubia wakazi wa Msoga katika Kmapeni zake leo  Jumapili Septemba 28,2025, Dk. Samia amesema  uwanja huo ni sehemu ya shukrani kwa Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye anatoka katika kijiji hicho.

“Hii ni kama shukrani yetu kwa utumishi wa Rais wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete. Mengi tumeyapa jina la Kikwete, lakini sio Msoga. Hapa hatukufanya kitu, kwa hiyo uwanja ule tutauweka Msoga kuonesha shukrani yetu kwa Rais wa awamu ya nne,” amesema Dk. Samia.

Aidha, ameahidi kuendelea kusogeza huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi pamoja na kukamilisha uhakiki wa madai ya fidia kwa baadhi ya wakazi wa Msata waliopisha miradi ya maendeleo katika eneo hilo.

Dk. Samia ametoa ahadi hizo akiwa njiani kuelekea mkoani Tanga kuendelea na mikutano yake ya kampeni.

About the author

Alex Sonna