Mamia ya wananchi wa Mchinga, Mkoani Lindi leo Alhamisi Septemba 25, 2025 wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea na Mikutano ya hadhara ya Kampeni zake kuelekea uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Sehemu ya wananchi wa Mchinga, mkoani Lindi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 25 Septemba, 2025.
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Mchinga katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM, mkoani Lindi tarehe 25 Septemba, 2025.
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mchinga Salma Kikwete mara baada ya kuhutubia wananchi wa Jimbo hilo mkoani Lindi tarehe 25 Septemba, 2025.
Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Mchinga mkoani Lindi tarehe 25 Septemba, 2025.