Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
MGOMBEA mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameendelea kufanya mikutano ya kampeni kuelekea Uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu ambapo leo amehutubia maelfu ya wananchi Jimbo la Mufindi mkoani Iringa.
Dk.Nchimbi amefanya mkutano wa kwanza wa hadhara wa kampeni katika kata ya Ifwagi,ndani ya Jimbo la Mufindi Kaskazini mkoa wa Iringa baada ya kuhitimisha mikutano yake ya kampeni mkoani Njombe.
Akiwa katika mkutano huo amenadi sera na Ilani ya CCM ya mwaka 2025 – 2030 sambamba na kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani.
Pia Dkt.Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe,Wagombea Ubunge wa mkoa huo pamoja na Madiwani.
Kwa upande wao wa wananchi wa Jimbo hilo
wamemuahidi Dk.Nchimbi kwamba katika Uchaguzi mkuu watapiga kura za ushindi wa kshindo kwa Mgombea Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29,2025