Featured Kitaifa

DKT. STERGOMENA TAX AZINDUA KAMPENI ZA CCM KATA YA KANDAWE

Written by Alex Sonna

 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Mlezi wa Kata ya Kandawe Wilaya ya Magu, tarehe 17 Septemba 2025, amezindua Kampeni za Uchaguzi katika Kata hiyo ambapo amemnadi na kumkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi Mgombea Udiwani wa Kata ya Kandawe ndugu Lucas Bomoa na viongozi wa Chama katika Kata hiyo.

Katika Mkutano huo, Dkt, Stergomena Tax, ametoa wito kwa wana CCM kushirikiana pamoja kufanya Kampeni mtu kwa mtu, nyumba kwa nyumba, Kitongoji kwa Kitongoji na Kijiji kwa Kijiji ili kukiletea ushindi Chama cha Mapinduzi kiendelee kushika dola.

Pamoja na kumwombea Kura za Udiwani ndugu Bomoa, Dkt. Stergomena Tax, pia alitumia hadhira ya Mkutano huo kumnadi na kumwombea kura Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ndugu Boniventura Kiswaga anaegombea nafasi ya Ubunge wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Magu ili kuendelea kufaidika na uongozi unaowajali Wananchi.
Akizungumza na Wananchi, Dkt. Tax aliwataka Wana CCM kuyaelezea mafanikio yaliyopatikana katika Serikalinya ya Awamu ya Sita katika maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na Shule za Sekondari, Shule za Msingi, vituo vya Afya, Zahanati, barabara, madaraja, umeme vijiji vyote, bila kusahau miradi ya Kimkakati kama Miradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, reli ya mwendo kasi SGR, Daraja la Busisi, miradi yote hii ina manufaa makubwa kiuchumi na kijamii kwa Taifa letu ikiwa ni pamoja na Wilaya ya Magu na Kata yetu ua Kandawe.
Aidha, kabla ya kuhitimisha Hotuba yake, Dkt. Tax amewaomba Wananchi kujitokeza siku ya kukipigia Kura 29 Octoba 2025 na kutumia haki yao ya kikatiba na kuwapigia Kura Wagombea kutoka Chama cha Mapinduzi CCM kupitia mafiga matatu yaani Rais, Mbunge, Diwani ili kuendelea kunufaika na maendeleo yaliyoletwa na yatakayoletwa na Chama hicho kupitia Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

About the author

Alex Sonna