Featured Kitaifa

WAKULIMA WA TUMBAKU TABORA KUANDIKISHWA KABLA YA MSIMU WA KILIMO

Written by Alex Sonna

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege,akizungumza kwenye kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WADAU wa zao la Tumbaku nchini wamekutana jijini Dodoma na kuweka mkakati wa pamoja wa kuhakikisha wakulima wanapata bima ya zao hilo kupitia vyama vyao vya ushirika, ili kuwalinda dhidi ya majanga na hasara zinazoweza kuathiri uzalishaji.

Kikao hicho maalum kimewaleta pamoja Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Konsotia ya Bima za Kilimo (TAIC), taasisi za kifedha na wakuu wa wilaya za mkoa wa Tabora.

Lengo  la mkutano huo ulikuwa  kutafuta suluhu ya changamoto zinazowakabili wakulima wa tumbaku, hususan uhakika wa kipato wanapokumbana na majanga ya asili au mazingira yasiyotabirika, pamoja na utoroshaji wa mazao.

Akizungumza kwenye kikao hicho Lleo Septemba 17,2025 jijini Dodoma, Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege, amesema kuwa hatua hiyo ni mwanzo wa kuhakikisha kila mkulima wa tumbaku anakuwa na bima ya mazao kabla ya kuanza msimu mpya wa kilimo.

“Usajili wa wakulima wa tumbaku utaanza mara moja na takwimu zao zitakusanywa kwa manufaa ya wakulima wenyewe, taasisi za kifedha na kampuni za bima. Tunataka mfumo wa bima uwe na tija na kulinda kipato cha mkulima,” amesema  Dkt. Ndiege.

Aidha ameongeza kuwa bima kwa wakulima kwa sasa ni jambo la lazima kwa kuwa inawalinda wanapokumbwa na majanga, huku akibainisha kuwa Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kila mkulima anakuwa na bima ya mazao.

“Kupitia ushirika, wakulima wataweza kupata huduma ya bima kwa urahisi zaidi, huku taasisi za kifedha na kampuni za bima zikihakikisha mfumo huo unakuwa endelevu.”amesema Dkt. Ndiege.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Dkt. Khamis Mkanachi, amesema kuwa usajili na bima kwa wakulima ni hatua ya kudhibiti mianya ya utoroshaji wa tumbaku na kuhakikisha mkulima anakua na maslahi ya moja kwa moja kupitia chama chake cha ushirika.

Dkt.Mkanachi, amesema kuwa usajili wa wakulima ni hatua muhimu na ya haraka, kwani bila ya zoezi hilo uhalali na utambuzi wa wakulima unabaki kuwa fumbo.

 “Kukamilika kwa usajili huo kutasaidia kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa tumbaku, kwa kuwa mkulima atakayekopeshwa na benki kupitia chama cha ushirika atalazimika kuuza tumbaku yake kupitia chama hicho na si vinginevyo.”amesema Dkt.Mkanach

Wadau hao wameeleza kuwa bima ya mazao ni nguzo muhimu katika kulinda ustawi wa wakulima na kuongeza tija ya kilimo, jambo litakalosaidia sekta ya tumbaku kuchangia ipasavyo katika pato la taifa.

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege,akizungumza kwenye kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.

Kamishna wa Bima  Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) – Dkt. Baghayo Saqware,akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.

 Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Dkt. Khamis Mkanachi,akichangia mada  wakati wa kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dkt Gerald Mongella,akichangia mada  wakati wa kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.

Wadau mbalimbali wakisikiliza hotuba ya Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege,(hayupo pichani) wakati wa  kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.

About the author

Alex Sonna