MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amepokewa kwa kishindo alipowasili kwenye uwanja wa Polisi,Longido kwa ajili ya kuwahutubia Wananchi kwenye mkutano wa kampeni leo Ijumaa Septemba 12,2025.
Mara baada ya kuwasili ,Balozi Nchimbi alikaribishwa kwa kuvalishwa vazi la heshima kutoka kwa viongozi wakuu wa kimila wa Kabila la Kimasai (Malaigwanani).