MGOMBEA mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi, amewasalimia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi mkoani Arusha na kuwaomba kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Dk. Nchimbi akizungumza hayo leo, Septemba 12, 2025, wakati akiendelea na mikutano yake ya kampeni kwa ajili ya kunadi Ilani ya CCM pamoja na kuwanadi wagombea wa chama hicho katika nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani.