Featured Kitaifa

TANZANIA NA OMAN KUIMARISHA UHUSIANO WA KIBIASHARA

Written by Alex Sonna

 

 

Katibu Mkuu wizara ya Viwanda na Biashara,Dkt. Hashil Abdallah akimsikiliza Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Nyama (Union Meat Group) Pius Shikoneke akiwa anatoa maelezo kuhusu hatua mbalimbali za uchinjaji na ufungashaji wa Nyama wakati wa ziara ya ujumbe wa Omani uliongozwa na Mkuu wa msafara kutoka Omani,Dkt. Salem Suleym bin Salih Al Junaib (wapili kushoto) Septemba 7, 2025 Kibaha mkoani Pwani.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,Dkt. Hashil Abdallah (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Msafara kutoka Omani, Dkt. Salem Suleym bin Salih Al Junaib (kushoto) baada ya kutembelea kiwanda cha Nyama kilichopo Kibaha ( Union Meat Group) kuangalia hatua mbalimbali za uchinjaji na ufungashaji wa Nyama wakati wa ziara ya ujumbe huo kutoka Omani Septemba 7, 2025 Kibaha, Pwani.

……

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdalah amesema ujio wa ujumbe wa wafanyabishara kutoka nchini Oman utazidi kuitangaza Tanzania kimataifa hususani katika sekta ya viwanda na biashara hali itakayoongeza wawekezaji kutoka nje ya Tanzania

‎Dkt Abdallah ameyasema Septemba 07, 2025 wakati wa Ziara ya Ujumbe huo katika Kiwanda cha Union Meat Group kinachojihusisha na uchakataji wa nyama ya mbuzi na kondoo pamoja na Kongani ya Viwanda ya Kasasa (KAMAKA ) vilivyopo Mkoani Pwani.

Naye, Mjumbe wa Baraza la Nchi na Mwenyekiti wa Chama cha Biashara na Viwanda cha Oman Mkoa wa Al Wusta na Kiongozi wa Ujumbe huo
Dkt. Salem bin Salim Al-Junaibi amesema ujumbe huo ulivutiwa na kufurahishwa na uwezo wa Kiwanda cha Union Meat kwa kuzingatia viwango vya juu kutoka kwenye usafi na weledi wa wafanyakazi hadi uzingatiaji wa viwango vya Halal.

“Ushirikiano huu unakuja kwa wakati unaofaa, tunapobadilisha uchumi wetu na kuimarisha ushirikiano katika biashara na uwekezaji wa kimkakati katika vifaa, bandari, kilimo, utalii, nishati pamoja na usalama wa chakula.” Bw. Al-Junaibi alisema

‎Akizungumza kwa niaba ya ujumbe kutoka Oman Bw. Zahran Al Aras ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji na kuahidi kuendelea kununua nyama kutoka Tanzania kwa kuwa ina radha nzuri.

‎Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bi Mariam Gw’hwani ameuhakikishia ujumbe huo Kuwa Union Meat itaendelea kuzingatia viwango vya kimataifa vya afya, usafi, na utii wa Halal na kuwa Kiwanda chake kina uwezo wa kuchinja na nyama ya mbuzi na kondoo 3500 wanachinjwa kiwandani hapo kwa siku na

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima nchini TCCIA Bw. Oscar Kissanga amesema faida ya ujio wa ujumbe huo nchini kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizo na Kuwa taasisi yake iko tayari kutumia fursa zitakazotokana na uhusiano huo.

‎Ujumbe huo wa wafanyabishara zaidi ya 15 umetembelea pia eneo la uwekezaji wa viwanda la KAMAKA lililopo Kibaha Pwani huku ukitarajiwa kuwepo nchini kwa siku tano na kutembelea miradi mbalimbali.

 

About the author

Alex Sonna