Mkuu wa Wilaya ya Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale ,Grace Kingalame akiongea katika hafla ya uzinduzi wa stendi ya mabasi ya Ikangala ambayo imejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Barrick Bulyanhulu
Mkuu wa Wilaya ya Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale ,Grace Kingalame akiongea katika hafla ya uzinduzi wa stendi ya mabasi ya Ikangala ambayo imejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Barrick Bulyanhulu
Mwakilishi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu, David Magege akiongea katika hafla ya uzinduzi wa stendi ya mabasi ya Ikangala ambayo imejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Barrick Bulyanhulu
*
Nyang’hwale: Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umefanikisha kuondoa kero ya muda mrefu ya kutokuwepo stendi ya mabasi kwenye Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, ambapo kupitia fedha za uwajibikaji wa jamii (CSR) kwa kushirikiana na Halmashauri hiyo umejenga stendi ya kisasa ya Ikangala kwa gharama ya shilingi milioni 299.9.
Hafla ya uzinduzi wa stendi hiyo imefanyika wilayani humo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wananchi, wafanyakazi wa Barrick ambapo mgeni alikuwa ni Mkuu wa wilaya hiyo, Grace Kingalame.
Akifungua stendi hiyo, Grace Kingalame amesema miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na wawekezaji ni matunda ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki kwa uwekezaji nchini.
Kingalame amewataka wananchi , wafanyabiashara pamoja na wadau wote wa usafirishaji kutumia fursa ya stendi katika kujikwamua kiuchumi.
“Natoa rai kwa wananchi na wadau wote wa usafirishaji waweze kutumia fursa ya uwepo wa stendi hii kujikwamua kichumi kupitia biashara mbalimbali zinazotokana na mahitaji ya utoaji wa huduma kwa wasafiri,” amesema.
Awali Akisoma Taarifa ya ujenzi, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Bruno Marco amesema ujenzi huo unatekelezwa kwa awamu kwa kutumia mfumo wa mkandarasi kwa baadhi ya kazi na wataalamu wa ndani (Force Akaunti), na hadi sasa mradi umefikia asilimia 85.
“Ujenzi wa Stendi ya Ikangala unajumuisha miundombinu mbalimbali ikiwemo choo cha stendi, eneo la kuegesha magari ya abiria, jengo la abiria, jengo la huduma ya chakula, jengo la mkusanya mapato, kizimba cha kuhifadhia taka, fremu za maduka, jengo la polisi, na Mgahawa”, amefafanua.
Mwakilishi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika hafla hiyo, David Magege ambaye ni Afisa Uhusiano wa Jamii katika mgodi huo ameipongeza Halmashauri ya Nyang’hwale kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa mradi huo na miradi mingine inayoendelea kutekelezwa na fedha za CSR na kutoa wito kwa kamati ya maendeleo ya jamii (CDC) kuendelea kuibua miradi yenye tija inayolenga kuleta maendeleo na kunufaisha wananchi.
Mwenyekiti wa Wafanyabishara Wadogo yaani Machinga wa wilaya hiyo Bi. Dorcas Hussein akiongea kwa niaba ya wafanyabiashara na wananchi amesema wamefurahishwa kufunguliwa na kuanza kutumika kwa stendi ya mabasi Ikangala kwa kuwa utawapatia fura ya kujiendeleza kibiashara sambamba na kujikwamua kiuchumi,”Tunashukuru Serikali na Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kutuletea miradi ya maendeleo”, amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale ,Grace Kingalame akiongea katika hafla ya uzinduzi wa stendi ya mabasi ya Ikangala ambayo imejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Barrick Bulyanhulu
Mwakilishi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu , David Magege akiongea katika hafla ya uzinduzi wa stendi ya mabasi ya Ikangala ambayo imejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Barrick Bulyanhulu
Sehemu ya miundombunu katika stendi ya Ikangala

Sehemu ya wananchi wakiwa katika hafla hiyo