Featured Kitaifa

WACHAMBUZI WATAKIWA KUFANYA TAFITI KABLA YA KUCHAMBUA MIRADI YA SERIKALI

Written by Alex Sonna
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wachambuzi wa masuala mbalimbali wamehimizwa kufanya tafiti ya kutosha kabla ya kufanya chambuzi zao ususani linapokuja suala la utekelezwaji wa miradi inayosimamiwa na Serikali ili kuepusha upotoshaji kwenye jamii
Hayo yamesemwa leo Agosti 30, 2025 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPPC), David Kafulila wakati wa mdahalo maalum ulioratibiwa na Jukwaa la Wachambuzi, ambao ulikuwa na mada isemayo mwenendo wa uchumi wa awamu ya sita na nafasi ya sekta binafsi na umma katika ujenzi wa uchumi jumuishi.
Aidha Kafulila amesema katika maendeleo ya nchi yoyote duniani uadilifu ni suala muhimu na la kuzingatiwa sana ili kufikia malengo ya kitaifa.
Amesema ni muhimu zaidi kila mwananchi kuzingatia suala la uadilifu katika sekta zote zinazogusa uchumi wa taifa, huku akihadharisha kwamba rushwa na matumizi mabaya ya malighafi za taifa zinarudisha nyuma kasi ya maendeleo.
“Ni muhimu na lazima kuwa na watu wenye maarifa, uadilifu na bidii. Hivi vitu vitatu ndio vinaamua uimara wa watu kuanzia ngazi ya familia ipande kwenye kijiji, kata mpaka taifa”. Amesema Kafulila
Baadhi ya wachambuzi wamesema mafunzo hayo yatawasaidia katika kutekeleza majukumu yao











About the author

Alex Sonna