Featured Kitaifa

MAJALIWA: ELIMU YA WATU WAZIMA NI ZANA YA MAENDELEO ENDELEVU

Written by Alex Sonna

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza, kwenye kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Agosti 25.2025. (Pichana Ofisi ya Waziri Mkuu)

………….

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema elimu ya watu wazima sio tu elimu ya masomo ya kawaida, bali ni zana muhimu ya maendeleo endelevu, kwani inachangia kipato, ustawi wa kijamii, afya na ushiriki wa kiraia.

ameongeza kuwa uzoefu duniani unaonesha kwamba elimu ya watu wazima ni chombo muhimu cha maendeleo ya kijamii, kiuchumi na binafsi.

Amesema hayo leo Jumatatu (Agosti 25, 2025) alipofungua kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Elimu si tukio la muda bali ni safari endelevu ya kujifunza katika maisha yote, elimu ya Watu wazima si kwa ajili ya watu wazima pekee, bali hata kundi la vijana wanaweza kujiunga na kunufaika na program mbalimbali za ujuzi zinazotolewa na taasisi hiyo”.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inatambua kwamba katika kipindi cha nusu karne iliyopita, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imepiga hatua kubwa na kutoa mchango wa kipekee katika maendeleo ya Taifa.

“Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imekuwa ikishauri Serikali kwenye maeneo ya kisera na kitaalamu katika masuala ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi iliyosaidia kuwafikia Watanzania wengi zaidi waliokuwa hawajapata fursa ya elimu ya msingi”.

Mheshimiwa Majaliwa ameielekeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuhakikisha wanaongeza wigo wa upatikanaji wa elimu ya watu wazima ikiwemo kuwafikia makundi yote nchini hasa maeneo yaliyo pembezoni na yenye changamoto za kijamii na kijiografia.

Pia, ameiagiza Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kwa kushirikiana na wadau waendelee kufanya tafiti za mara kwa mara kuhusiana na elimu ya watu wazima ili kubaini changamoto zinazojitokeza na kuandaa suluhisho bunifu linaloendana na mahitaji halisi ya jamii.

Naye, Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima imekuwa ikitekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati ikiwemo mradi wa SEQUIP (Secondary Education Quality Improvement Project) ambapo umefanikiwa kuwarejesha wasichana 13,272 katika mfumo wa elimu katika kipindi cha miaka mitano.

Amesema kuwa mradi mwingine ni IPOSA (Integrated Programme for Out-of School Adolescents) ambao umewezesha kuwajengea uwezo vijana 10,000 walioko nje ya mfumo rasmi katika maeneo ya stadi za maisha, ujasiriamali na ufundi wa awali

Kwa Upande wake Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Prof. Philipo Sanga amesema kuwa Taasisi hiyo inajivunia mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita hasa katika kuboresha mifumo ya elimu ikiwemo sera ya elimu jumuishi ambayo inagusa makundi yote pasipo ubafuzi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo Waziri wa Elimu Mstaafu, Dkt. Nicholas Kuhanga kwa kutambua mchango wake wa maendeleo kwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Programu zake, katika kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Agosti 25.2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea tuzo kwa naiba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, ya kutambua mchango wake uliyotukuka katika elimu jumuishi na mbadala pamoja na kutoa fursa kwa wanafunzi wa kike ambao hawakuweza kumaliza masomo yao kutokana na sababu mbalimbali, kwenye kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mwalimu mbunifu Frank Mselu (wapili kutoka kulia), kutoka kwenye mradi wa kuwajengea vijana walioko nje ya mfumo rasmi wa elimu stadi za maisha, ujasiriamali na ufundi wa awali, kwenye kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Agosti 25.2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Profesa Philipo Sanga (katikati), kwenye kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Agosti 25.2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia picha iliyochorwa na Iclam Mfaume wa Swergen Art, kwenye kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Agosti 25.2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishika mpira uliyotengenezwa na Taasisi ya Karibu Tanzania Organization, kwenye kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Agosti 25.2025. Kutoka kulia ni Mnufaika Tulizo Matwebe na Mkufunzi Johnither Kabunga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua mfumo wa kupata taarifa kuhusu elimu ya watu wazima (OSMIS), kwenye kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Agosti 25.2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About the author

Alex Sonna