Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango na ujumbe wake wakipata maelezo ya utendaji kutoka kwa Meneja wa Barrick nchini, Dk. Melkiory Ngido kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Twiga, Casmir Kyuki.
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango na ujumbe wake wakipata maelezo ya utendaji kutoka kwa Meneja wa Barrick nchini, Dk. Melkiory Ngido kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Twiga, Casmir Kyuki.
Meneja wa Barrick nchini, Dk. Melkiory Ngido akifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa kikao hicho
Meneja wa Barrick nchini Dk. Melkiory Ngido akiongea na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa kampuni na udhamini wa mkutano huo
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa kikao

Wageni mbalimbali wametembelea banda la maonesho la Barrick na kupokelewa vizuri na kupatiwa maelezo kuhusiana na utendaji wa kampuni na mafanikio yaliyopatikana kutokana na uwekezaji wake
**
Serikali imeipongeza Barrick-Twiga kwa uendeshaji wa shughuli zake nchini kwa ufanisi na kuwa kielelezo cha ubia wa mfano wa kampuni binafsi na Serikali wenye mafanikio makubwa katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu wa Rais, Dk. Philipo Mpango, baada ya kutembelea banda la maonesho la Barrick-Twiga kwenye kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma 2025 kinachoendelea jijini Arusha kwenye hoteli ya AICC na kupata maelezo ya utendaji wa kampuni kutoka kwa Meneja wa Barrick nchini, Dk.Melkiory Ngido.
Dk.Ngido alieleza kuwa ubia wa Barrick-Twiga unaendelea kuleta tija na ufanisi nchini katika kuchangia uchumi wa Taifa sambamba na kutekeleza miradi mikubwa yenye tija kwenye jamii zinazozunguka migodi na sehemu nyinginezo ambayo inaendelea kubadilisha maisha ya wananchi kuwa bora.
Alisema Barrick-Twiga itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi nchini kwa kasi.
Akiongea baadaye na waandishi wa habari kuhusiana na kudhamini na ushiriki wa kampuni katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma 2025, Dk. Ngido, alisema Barrick inaamini kuwa mafanikio ya kiuchumi yatapatikana kutokana na ushirikiano wa karibu wa wadau wote waliopo katika sekta ya biashara na huduma kwa upande wa Serikali na sekta binafsi.
“Kikao hiki kwetu ni cha muhimu kwa kuwa kinakutanisha viongozi wa Serikali na watendaji wa taasisi za Umma na kubadilishana uzoefu na kujengewa uwezo hivyo Barrick kama mmoja wa wawekezaji wakubwa nchini inafurahi kushirikishwa katika kikao cha mwaka huu kama mwekezaji ambaye anafanya kazi kwa ubia na Serikali wenye mafanikio makubwa’’,alisema Dk.Ngido.
Alisema tangu mwaka 2019 Barrick ilipoanza kuendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali, ubia huu umekuwa kielelezo na mfano wa kuigwa kwa kuwa umeonyesha kuleta mafanikio, kunufaisha pande zote mbili sambamba na kunufaisha wananchi.
Kupitia migodi yake ya dhahabu ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi, kampuni imeweza kuchangia pato la Serikali kwa kiasi kikubwa kupitia kodi, tozo mbalimbali, gawio, mishahara, malipo kwa wazabuni wa ndani na kufanikisha miradi mbalimbali hususani katika sekta ya afya, elimu na kuboresha miundombinu kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR).
Alisema mwaka huu Kampuni ya Barrick-Twiga ilitoa gawio la shilingi bilioni 93,6 kwa Serikali ya Tanzania na kutunukiwa tuzo ya kwanza katika kundi la makampuni ambayo Serikali ina hisa chache ambapo pia katika miaka ya nyuma imefanikiwa kutoa gawio nono kwa Serikali.
Hivi karibuni Barrick Mining Corporation, ilitoa mrejesho wa mkakati endelevu wa miaka sita katika uendeshaji wa shughuli zake katika nchi mbalimbali duniani ambapo ilidhihirisha kuendeleza miradi ya ukuaji wa msingi iliyoundwa kuleta thamani ya muda mrefu kwa wadau wote kupitia ushirikiano wa kweli.
Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Makamu wa Rais ,Dk. Philip Mpango,aliyemwakilisha Rias Samia Suluhu Hassan ,Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, alisema mkutano wa mwaka huu ni tofauti na miaka ya nyuma mbali na kushirikisha watendaji wakuu wa taasisi za umma umeshirikisha watendaji wa makampuni na taasisi binafsi ambazo Serikali ina hisa chache.
Mchechu alisema mfumo huu wa kukutanisha wakuu wa taasisi binafsi na Serikali utasaidia kubadilishana uzoefu ili kuweza kwenda pamoja katika mchakato wa kukuza biashara na uboreshaji huduma kwa wananchi sambamba kukuza uchuni wananchi kuendana na malengo ya dira ya taifa ya 2025-2050 iliyozinduliwa karibuni.