Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi majiko yanayotumia Nishati Safi kwa Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyofanyika leo Agosti 22,2025 jijini Dodoma.
….
-Asema REA inabeba kikamilifu ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia
-Asema miradi yote inayosimamiwa na REA hukamilika kwa wakati na kwa ubora
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kukamilisha lengo la usambazaji Umeme katika Vijiji 12,318 Nchini na kwa umahiri wake katika kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
Ametoa pongezi hizo Agosti 22, 2025 Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi majiko yanayotumia Nishati Safi kwa Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
“REA mmefanya kazi kubwa, tunawapongeza kwa kuibeba vyema ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Nishati Safi ya Kupikia sambamba na kukamilisha kwa wakati lengo la kufikisha umeme katika vijiji vyote 12,318 na sasa mnasambaza umeme vitongojini,” alipongeza Mhe. Dkt.Biteko.
Aliipongeza Bodi ya Nishati Vijijini (REB) chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu kwa umahiri wake katika katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kasi na viwango sambamba na kumpongeza Mtendaji Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy kwa kusimamia vyema watendaji walio chini yake.
Alibainisha kuwa Wizara ya Nishati inao utaratibu wa kupima utendaji wa kila taasisi inayoisimamia na kwamba REA ni taasisi ambayo imefanya vizuri mara tatu mfululizo katika tathmini hiyo ya utendaji wa taasisi ambayo hufanyika kila baada ya miezi mitatu.
“Katika robo ya kwanza ya upimaji wa utendaji REA ilishinda nafasi ya kwanza, robo iliyofuatia REA ilichukua nafasi ya pili na robo hii iliyomalizika hivi karibuni REA imeshika nafasi ya kwanza kwa taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Nishati, kazi mnayofanya imewezekana kwasababu ya utulivu wa taasisi, mnayo Bodi nzuri na uongozi mzuri,” alibainisha Mhe. Dkt. Biteko.
Aliongeza kuwa miradi yote inayosimamiwa na REA inakamilika kwa wakati na kwa ubora mzuri na kwamba hajawahi kupokea malalamiko yoyote kutoka kwa wafadhili wa miradi na mara zote wamekuwa wakimpatia sifa njema za utendaji wa Wakala.
“Nampongeza Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy kwa uongozi wake amewafanya watumishi wa REA wajione wa daraja la juu, hajawagawa kwa makundi hana wapambe ndio maana huwezi kusikia kelele, tuendelee kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia vyema miradi tuliyokabidhiwa,” alisema Mhe.Dkt. Biteko.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu alisema Wakala unaendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa vitendo.
“Ombi langu zoezi hili itapendeza na kuleta matokeo chanya endapo taasisi zote zitatoa majiko haya kwa watumishi; hii italeta chachu kwa Wizara zingine na taasisi mbalimbali kufanya vivyo hivyo na itaongeza kasi ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais ya kuhakikisha 80% ya Watanzania wanahamia kutumia Nishati Safi ifikapo mwaka 2034 na hili linawezekana,” alisema Balozi Kingu.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Nishati Safi ya Kupikia, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy alimshukuru Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa miongozo yake ya namna bora ya kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ili kufikia lengo la 80% ifikapo mwaka 2034.
Mhandisi Saidy aliainisha mikakati mbalimbali inayoendelea kutekelezwa kupitia REA na alitaja baadhi ya miradi ikiwemo kujenga mifumo ya gesi asilia Lindi na Pwani na kwamba hadi sasa wananchi 460 wamefikiwa kati ya 980 waliolengwa, kufunga mifumo katika Jeshi la Magereza ambapo magereza yote 129 yamefikiwa sambamba na kufunga mifumo katika kambi 22 za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Mbali na miradi hiyo, Mhandisi Saidy alisema REA imeliwezesha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kiasi cha shilingi bilioni 3 kujenga mtambo wa kuzalisha mkaa mbadala maarufu kama ‘rafiki briquettes’, majiko banifu 200,000 vijijini kusaidia wananchi ambao ni ngumu kufikiwa na nishati safi zingine.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi majiko yanayotumia Nishati Safi kwa Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyofanyika leo Agosti 22,2025 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi majiko yanayotumia Nishati Safi kwa Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyofanyika leo Agosti 22,2025 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi majiko yanayotumia Nishati Safi kwa Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyofanyika leo Agosti 22,2025 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi majiko yanayotumia Nishati Safi kwa Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyofanyika leo Agosti 22,2025 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi majiko yanayotumia Nishati Safi kwa Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyofanyika leo Agosti 22,2025 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akimkabidhi jiko Mtumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Bi. Magdalena Muhazi wakati wa hafla ya kukabidhi majiko yanayotumia nishati safi kwa watumishi iliyofanyika jana katika viwanja vya Wakala huo, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akimkabidhi jiko Mtumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Ernest Makale wakati wa hafla ya kukabidhi majiko yanayotumia nishati safi kwa watumishi iliyofanyika jana katika viwanja vya Wakala huo, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi majiko yanayotumia Nishati Safi kwa Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyofanyika leo Agosti 22,2025 jijini Dodoma.