Featured Kitaifa

TBS YASHIRIKI MAONESHO YA KITAIFA NANENANE

Written by Alex Sonna

 

MENEJA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati, Mwalimu Hamis Sudi Mwamasala,akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la TBS wakati wa Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma.

Na Alex Sonna, Dodoma
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema litaendelea kulinda afya za Watanzania kupitia udhibiti wa ubora wa bidhaa kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya masuala ya viwango moja kwa moja kupitia njia mbalimbali ikiwamo Maonesho.
Meneja wa TBS Kanda ya Kati, Hamis Sudi Mwanasala, amesema hayo leo Agosti 5 ,2025 Kwenye maonesho ya wakulima Nanenane -Nzuguni na kueleza kuwa Shirika hilo kama taasisi ya umma lina jukumu la kuhakikisha bidhaa zote sokoni zinakuwa salama na zenye viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.
“Tunatumia maonesho kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa viwango na kutumia bidhaa zilizo thibitishwa  ubora wake na TBS. Kupitia maonesho ya nanenane, wakulima na wajasiriamali wanapata nafasi ya kujifunza moja kwa moja kutoka kwetu kuhusu namna bora ya kuzalisha bidhaa bora na salama  zenye kuleta ushindani sokoni,” amesema Mwanasala.
Amesema wananchi wengi wanaofika kwenye banda la TBS wamekuwa wakitoa pongezi na kueleza kuwa shirika hilo limekuwa msaada mkubwa katika kuhakikisha bidhaa hafifu  zinadhibitiwa kabla ya kufika sokoni.
Mwanasala ametoa wito kwa wakulima, wajasiriamali na wananchi wote kutembelea banda la TBS lililopo katika maonesho  ili kupata elimu na huduma, akibainisha kuwa uelewa wa viwango ni msingi wa kujenga taifa lenye uchumi wa viwanda na bidhaa ubora na salama kwa watumiaji.
Kwa upande wake, Afisa Udhibiti Ubora wa TBS Kanda ya Kati, Bw. Daniel Marwa, amesema huduma zinazotolewa kwenye maonesho hayo ni pamoja na usajili wa majengo  ya chakula na Vipodozi ambao hufanyika kupitia mfumo.
Marwa amesema huduma hiyo inasaidia kuimarisha ubora na usalama wa chakula na Vipodozi ili kulinda afya ya walaji, hatua itakayoongeza ushindani wa bidhaa ndani na nje ya nchi.
Aidha, TBS imekuwa ikitoa mafunzo kwa wazalishaji  kuhusu umuhimu wa kupata alama ya ubora.
“Tunahamasisha wakulima kuongeza thamani ya mazao yao ili kuweza kupata masoko ya ndani na nje,” alisisitiza Marwa.

MENEJA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati, Mwalimu Hamis Sudi Mwamasala,akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la TBS wakati wa Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma.

AFISA Udhibiti Ubora wa TBS Kanda ya Kati, Bw. Daniel Marwa,akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la TBS wakati wa Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma.

MENEJA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati, Mwalimu Hamis Sudi Mwamasala,akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 5,2025 katika banda la TBS wakati wa Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma.

About the author

Alex Sonna