MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe aliyemaliza muda wake,Dkt.Selemani Jafo, ameibuka kidedea katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupatakura 4,412 sawa na asilimia 76.
Waliokuwa wakichuana na Jafo katika kinyang’anyiro hicho ni Mpendu 835 sawa na asilimia 14,Chaurembo kura 309 sawa na asilimia 5,Janguo kura 153 sawa na asilimia 3 na Tabia kura 119 sawa na asilimia 2.