Featured Kitaifa

EWURA CCC YATAKIWA KUPELEKA ELIMU VIJIJINI

Written by mzalendo

Na Gideon Gregory, Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, ametoa wito kwa Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji (EWURA CCC), kuimarisha elimu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kufika maeneo ya vijijini ili kuongeza uelewa wa huduma hizo muhimu.

RC Senyamule ametoa rai hiyo leo Agosti 5,2025
leo Agosti 5, 2025 alipotembelea banda la Baraza hilo katika Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, Afisa uelimishaji na uhamasishaji kutoka baraza hilo Ligiko Lugiko amesema wanao mkakati wa mwaka 2024 mpaka 2034 kwaajili ya matumizi ya nishati safi.

“Matumizi ya nishati safi ya kupikia ni kitu halisi na na ni kitu kinawezekana sio vitu vya kufikilika, watu sasa wanaweza kupika kwa umeme, kwa gesi na hizi huduma zinapatikana na bei zinafikika kwa watanzania walio wengi,”amesema.

Aidha, ametoa rai kuwa Serikali inapohamasisha matumizi ya nishati safi watumiaji wahamasike kuhamia huko kwasababu ipo faida kubwa ya kiafya wanaipata ikiwemo kujiepusha na maradhi yatokanayo na matumizi ya nishati chafu.

Nao baadhi ya wananchi wamepongeza kwa elimu inayotolewa na baraza hilo kwani imeweza kuwafungua kifikra kutokana na yale waliyojifunza ikiwemo namna ya kuwasilisha malalamiko yao yanayohusiana na umeme, maji, gesi pamoja na petroli.

“Tunawapongeza EWURA CCC kwa elimu waliotupatia siku ya leo kwani hatukujua kama kuna watu wanaoweza kututetea kutokana na huduma tunayopatiwa, kwasababu unakuta muda mwingine tunapata changamoto mbalimbali lakini hatuna sehemu ya kuzupeleka,”wamesema.

EWURA CCC ilianzishwa chini ya kifungu namba 30 cha sheria ya EWURA, sura ya 414 ya sheria za Tanzania.

About the author

mzalendo