Featured Kitaifa

WANAFUNZI WAPATIWA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU

Written by mzalendo

Haki za binadamu zinaendana na wajibu,

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uchunguzi Mkuu Bw. Fadhili Muganyizi wakati akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari St Gabriel Tech walipotembelea Banda Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Bw. Muganyizi amesema kuwa watoto wana haki ya kuishi, kusikilizwa, kutoa maoni, kupata taarifa na haki ya kupata elimu

“Haki zote ni muhimu kuzipata na THBUB pia ina jukumu la kutoa elimu kwenu ili muweze kuzijua” amesema Bw. Muganyizi

Pia Bw. Muganyizi amewaeleza wanafunzi hao kuhusu wajibu wao wanapokuwa shuleni na katika Jamii kwani wao ni viongozi wa baadae.

“Pamoja na kuwa na haki ya kupata elimu, pia mna wajibu wa kusoma ili muweze kufaulu sambamba na kuheshimu jamii inayowazunguka ili kuwa viongozi bora wa baadae” amesema Bw. Muganyizia

Aidha, wanafunzi hao walielezwa pia majukumu ya THBUB ambapo pia walipata fursa ya kuuliza maswali kuhusu haki za binadamu na utawala bora .

Kwa wapande wake Anthonia Vendeline Mwanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka Shule hiyo ameishukuru THBUB kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo imewasaidia kutambua haki na wajibu wao sambamba na kuijua THBUB.

“Tumefurahi, asanteni sana” amesema Anthonia

About the author

mzalendo