Na.MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena ametoa rai kwa Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utendaji wa taasisi na programu mbalimbali zinazosimamiwa na Ofisi hiyo.
Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 02 Agosti, 2025 alipotembelea banda la Ofisi hiyo akiwa ameambatanan na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Stephen Nindi na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri katika Maonesho ya Naneane yanayofanyika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
“Wananchi wanauhitaji Mkubwa wa kufahamu shughuli zinazoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, hivyo kuna umuhimu wa kuandaa vipindi vya kuelimisha umma,” alieleza.
Maonesho ya Wakulima maarufu Nanenane yamebebwa na kauli mbiu isemayo: “Chagua Viongozi Bora, kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”