Featured Kitaifa

MWENGE WA UHURU WAKOSHWA NA MIRADI YA MAENDELEO KALIUA

Written by Alex Sonna

 

MKUU wa Wilaya ya Kaliua, Dk. Garald Mongela, amewaongoza maelfu ya wananchi wa wilaya hiyo kushiriki uzinduzi wa miradi ya kimkakati iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.

Katika mwaka huu Mwenge wa Uhuru umezindua, umeweka mawe ya msingi 

na umetembelea miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi 

2,275,516,058.60. 

Miradi hiyo ni uzinduzi wa Klabu ya Wapinga Rushwa Shule ya 

Sekondari Mwongozo, Ujenzi wa Nyumba ya Walimu ya Familia Mbili (Two in One) Shule ya Msingi Dk. Charles Msonde Shilingi 110,000,000 na Ujenzi wa Kitakasa Mikono Shule ya Msingi Dk. Charles Msonde Shilingi 10,205,313.

Miradi mingine ni Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) Zahanati ya Usigala Shilingi 72,400,000, Ujenzi wa Shule ya Sekondari Makingi 

Shilingi 603,890,563 na Mtambo wa Kutengeneza Barabara (Motor Grader) Shilingi 1,227,000,000.

Miradi mingine iliyozinduliwa ni Barabara ya Kuelekea Kituo cha Afya Ulyankulu (km. 2) Shilingi 1,603,040.00, Mradi wa Maji Kijiji cha Ulindwanoni Shilingi 219,817,142.60 na Mradi wa Kikundi cha Bodaboda (Boma Road) Shilingi 30,600,000.

About the author

Alex Sonna