Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa katika uwanja wa Mashujaa Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2025.

……. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 25 Julai 2025 ameongoza shughuli ya Kumbukizi ya Mashujaa waliopigana vita na kuitetea nchi ya Tanzania, Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa Mtumba jijini Dodoma, yalijumuisha ushiriki wa Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama nchini.
Katika shughuli hiyo, Rais Dkt. Samia aliweka Ngao na Mkuki katika Mnara wa kumbukumbuku ya Mashujaa ikiwa ni ishara ya kukumbuka na kuenzi Uzalendo wa Mashujaa waliokufa kwa ajili ya kulipigania Taifa la Tanzania. 
Viongozi wengine ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda aliweka Sime,  mwakilishi wa Mabalozi, Mhe. Halifa Abdurhaman Mohamed ameweka Shada la maua, Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Denis ameweka Upinde na Mshale pamoja na Mwakilishi wa Mashujaa waliopigana vita ya Kagera, Mhe. Balozi Brigedia Jenerali Francis Benard

      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu akishiriki maadhimisho ya Siku ya Mashujaa katika uwanja wa Mashujaa, Mtumba Jijini Dodoma leo, tarehe 25 Julai, 2025.    

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa katika uwanja wa Mashujaa Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2025.

            

About the author

mzalendoeditor