Featured Kitaifa

MAADHIMISHO YA 10 YA SIKU YA MWANI ZANZIBAR

Written by mzalendoeditor
Na Rahma Khamis Maelezo.
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Fatma Mbaruok Khamis amesema Serikali ina mpango wa kutengeneza chakula Cha kuku kupitia zao la mwani ili kuongeza thamani na kuwapatia tija wakulima wa zao hilo

Ameyasema hayo Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege katika maadhimisho ya 10 ya Siku ya Mwani Zanzibar.

Amesema kuwa sekta ya Mwani ni sekta muhimu hivyo ipo haja kwa wakulima, wadau na Serikali kwa ujumla kushirikiana kwa pamoja ili kutatua changamoto zinazojitokezs katika uzalishaji wa zao hilo
Ameongeza kuwa Serikali imechukua juhudi mbalimbali ikiwemo kuongeza bei na kugawa vifaa mbalimbali vya mwani ili kuongeza thamani katika zao hilo.
Aidha amefahamisha kuwa kupitia maadhimisho hayo  yataunganisha Taasisi binafsi, Serikali na wadau kwa ujumla katika mnyororo wa thamani wa sekta ya Mwani
 Mkurugenzi Idara ya Hifadhi na Mazao Baharini Dk Makame Omar Makame amesema kuwa Wizara ya Uchumi wa Buliuu imepanga kutenga matumizi Mazuri ya bahari  ili kila mdau anufaime wakiwemo wakulima wa mwani na kuepusha malalamiko
Aidha amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau  imefanya utafiti wa kugundua maeneo mbalimbali yenye uwezo wa kuzalisha mwani kwa wingi kuongeza thamani ya uzalishaji.
Nae Afisa Maendeleo ya Jamii Uchumi kutoka Taasisi ya Maisha Bora Foundation Joice John  amesema kuwa Taasisi yao imejikita kuwainua wananchi kiuchumi kupitia zao la mwani kwa kuwapatia mafunzo yatakayowasaidia kuzalisha zao hilo kwa wingi na kupata tija
Amefahamisha kuwa Kuna Umuhimu ya kuwapatia elimu ili kufahamu namna ya kuongeza  ubunifu, kusarifu zao hilo, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuwapatia boti ya kuvunia mwani ili kurahisisha 
Mmoja ya wakulima wa mwani kutoka Pwani Mchangani Mwanakheir Mussa Mhammed amesema changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa vifaa vya kusarifia zao hilo
Aidha ameiomba Wizara husika kupatiwa vifaa vya kusarifia mwani ikiwemo mashine na vifungashio ili kuongeza thamani ya zao hilo.
Katika maadhimisho hayo tunzo mbalimbali zimetolewa kwa wadau na wakulima wa zao hilo ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu “Kuimarisha mnyororo wa thamani ya Mwani ili kubotesha sekta ya Mwani”

About the author

mzalendoeditor